Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania inajivunia kufanya kazi kwa karibu na Nchi ya Rwanda kutokana na ukarimu mkubwa uliojengeka kwa muda sasa kwa Wananchi wa Nchi mbili hizo.

Makamu wa Rais amesema hayo leo alipokutana na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe.Eugene Kayihura wakati Balozi Kayihura alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kumuaga Makamu wa Rais Baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuhakikishia Balozi Kayihura kwamba Tanzania itaendelea kudumisha Uhusiano wa Nchi mbili hizi uliodumu kwa muda mrefu sasa katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo na kijamii hasa katika kuangalia fursa za kiuchumi pamoja na kuwa na uhusiano mzuri wa huduma ya Fedha kati ya Rwanda na Tanzania.

Mhe. Samia amesema muda umefika sasa kushirikiana pamoja kwa ajili ya kujenga Uchumi wa Mataifa haya, ambapo pia amempongeza Balozi Eugene Kayihura kwa Ushirikiano Mkubwa alioutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kipindi chake chote cha kazi hapa Nchini na kumtakia kila la Heri kokote aendako katika kituo chake kipya cha kazi.

Nae Nalozi Eugene Kayihura amemuhakikishia Makamu wa Rais kwamba, Rwanda itaendelea kukuza na kudumisha Ushirikiano na Tanzania katika pande zote za kimaendeleo na kuitakia Serikali ya Tanzania maandalizi mema ya mkutano wa SADC.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 09,2019 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 09,2019 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...