Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MFANYAKAZI wa Kampuni ya Simu ya Tigo Babati Hamis Singa (30) na wenzake wanne wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka saba likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Sh.milioni 26.

Washitakiwa wengine ni Jailos Joseph(33), makazi wa Arusha, Singa Mananga (32) mkazi wa Babati, Japhet Mkumbo (33) mkazi wa Babati na Omary Abdalah (33) mkazi wa Arushà.

Hamis ambaye ni raia wa Burundi na wenzake hao walipandishwa kizimbani mahakamani hapo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Ally Salim na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon.

Akisoma mashitaka hayo, Wakiki Simon alidai kati ya Januari na Julai mwaka huu katika sehemu tofauti Mkoa wa Manyara na Babati, washitakiwa wote walikula njama ya kutenda kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Ilidaiwa katika kipindi hicho na maeneo hayo, washitakiwa hao kwa ulaghai walijipatia Sh. 26, 432, 441 kupitia miamala ya wateja wa kampuni ya Vodacom na Airtel.

Siomon alidai katika kipindi hicho, washitakiwa hao walisambaza taarifa za uongo kupitia ujumbe wa maandisi usomekao 'tuma pesa kwa namba hii ' kwa lengo la kuudanganya umma wa Watanzania.

Katika shitaka lingine washitakiwa hao wanadaiwa kusambaza ujumbe ambao haujaombwa kupitia laini zao za simu za mkononi ambazo wamezisajiri kwa majina ya watu wengine. Pia wanadaiwa kusambaza ujumbe huo kwalengo la kujipatia fedha.

Mshitakiwa Hamisi pia anadaiwa akiwa mwajiriwa wa Tigo Babati, aliingilia taarifa za miamala ya fedha za mawakala wa Tigo kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Shitaka lingine, washitakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh. 26,432,441 wakati wakijua zilitokana na kosa la jinai ambalo ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwani Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi na imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu itakapotajwa tena. Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...