Na Ripota Wetu, Michuzi TV

MWENYEKITI mstaafu wa Chama cha soka Mkoa wa Shinyanga (Shirefa) Khamis Mgeja ambaye pia ni mdau mkubwa wa soka nchini amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuitisha mkutano wa wadau wa sekta ya michezo nchini ili kujadili changamoto na mstakabali wa maendeleo ya michezo mbalimbali hapa nchini ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa na watu walio wengi

Mgeja ambaye pia kada wa CCM ambaye kwa sasa amejikita katika sekta ya michezo hususani ile ya kukuza vipaji kwa vijana waliopo wilayani Kahama ameamua kumuomba Waziri Mkuu akiamini ni msikivu na mwanamichezo mzuri na kuongeza kama itampendeza na atakavyoona inafaa, afanye na yeye kuwaita wadau wa sekta ya michezo kama ambavyo amekuwa akifanya Rais Dk. John Magufuli kwa kuwaita wadau wa sekta mbalimbali na kuzungmza nao ili kutatua changamoto na kutoa maelekezo.

Mwenyekiti huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Kahama kuhusu mustakabali wa soka letu la Tanzania hasa katika mashindani mbalimbali ya kimataifa ambayo timu yetu ya taifa imeshiriki kuanzia ile ya chini ya miaka 17 pamoja na ile ya wakubwa ya Kombe la Mataifa ya Afrika sambamba na michuano hii ya kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

"Michezo kwa sasa ndio inachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi pamoja na kuona ajira kwa makundi makubwa ya vijana ambao kwa sasa ndio makundi makubwa ambayo yapo mitaani hayana ajira za kudumu na kupitia michezo wanaweza kujiajiri na kujipatia fedha zitakazo kuza maisha yao ya kila siku,"amesema Mgeja.

Amefafanua kuwa katika siku za hivi karibuni Rais Magufuli aliitisha mikutano kwa nyakati tofauti zikiwahusisha wadau kama vile wa madini na baadae wafanyabiashara, vikao hivyo vilikuwa na tija na mafanikio makubwa katika ujenzi wa Taifa. Baada ya wadau kupata nafasi ya kusema changamoto na mafanikio.

Aidha Mgeja amesema mkutano huo wa sekta ya michezo kama utaitishwa utatoa fursa ya wadau mbalimbali kutoa michango yao ya kimawazo na kujadili jinsi gani tutoke hapa tulipo kwenye aibu za mara kwa mara ili twende na kufika kwenye faraja hali ambayo tutapata wadau wengi na ikiwezekana wakawa na mawazo mazuri tofauti tofauti tukabadilishana mawazo na uzoefu na kufikia muafaka na kupanda daraja la michezo.

Hata hivyo Mgeja amewaomba Watanzania hasa wadau wa michezo wavute subira pamoja na kwamba tumeumia na tunaendelea kuumia baada ya matokeo ya mashindano ya watoto chini ya umri wa miaka 17 Afcon yaliyofanyika nchini kwetu na baadae Afcon ya wakubwa Misri hatuna sababu ya kutafuta mchawi wala kumtoa mtu kafara haitatusaidia chochote kuleta mabadiliko ya michezo na kama hatutajielekeza kuwekeza katika michezo Tanzania tutaendelea kuwa washiriki na wala shio washindani na tusitarajie kuvuna bila kupanda kama matunda pori.

"Hakuna njia ya mkato katika mafanikio yoyote yale bila kuwekeza katika soka na tatizo la watanzania tunataka matokeo mazuri kitu ambacho hakiwezekani hata ukitaka pepo lazima ufe kwanza.

“Msitake pepo bila kufa na inasikitisha tunataka maendeleo bila kuwekeza katika shule za mpira za watoto wadogo hapa nchini na hakuna njia nyingine yeyote ya kupata mafanikiom katika soka bila ya kuwea na shule za kufundisha watoto tangu wakiwa wadogo mapka wanapokuwea wakubwa na kusajiliwa na vilabu vingine”,amesema Mgeja.

Mgeja pia amewapongeza wachezaji na kocha wao Amunuke kwa pale walipofikia ni kweli vijana wetu uwezo wao ndipo ulipofikia katika mashindano ya Afcon na Misri ukweli utabaki pale pale. Ni kujidanganya kuwa tungeweza kufika kwenye robo fainali au nusu fainali na hatimaye fainali hayo yangekuwa maajabu makubwa ya dunia .

Amesema tumejifunza kuanzia Afcon ya watoto na wakubwa Misri tumeona wenzetu nchi zingine walivyowekeza kwa kiwango cha juu sana katika Academy Nchi kama Madagasca na Burundi na mfano wa kuigwa na sisi tujipange upya naimani tutafika pazuri penye faraja na sasa tumeingia katika mashindano ya Afcon ya wachezaji wa ndani na watanzania wanapenda kuona mabadiliko makubwa katika soka letu.

Amesema kuwa michezo kwa sasa hapa duniani ndio chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana ikiwa ni pamoja na kujenga afya za mwili na kama serikali itaongea na wadau mbalimbali kama ilivyo kwa sekta nyingine kunaweza kukaleta mabadiliko makubwa na hivyo kufanya nchi yetu kukua kwa kiwango cha juu katika sekta ya michezi kama ilivyo kwa nchini nyingine barani Afrika.

Mgeja pia amewapongeza ushirikiano mkubwa kama Taifa ulivyooneshwa katika mashindano ya Afcon chini ya umri wa miaka 17 yaliyofanyika nchini na Afcon ya wakubwa tuliyoshiriki Misri. Ushirikiano wa pamoja wa hali na mali ukiongonzwa na Rais Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais ,Waziri mkuu, Waziri wa michezo viongozi wa TFF.

Pia Mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji Taifa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Wadhamini mbalimbali wasani na Watanzania wote kwa ushirikiano huu tuliouonesha tunaweza kupiga hatua kubwa ya mafanikio kama walivyofanya nchi zingine Mfano Aljeria, Everycost, Cameroon, Nigeria, Misri, Tunisia na Senegal.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...