*Salumu Shamte apokea kijiti cha uenyekiti wa baraza la biashara (SADC) kutoka Namibia ahidi ushirikiano
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
TAASISI za sekta binafsi zimetakiwa kupambana na changamoto wanazokumbana nazo katika kujenga na kuimarisha uchumi badala ya kulalamika kwa kuwa hakuna njia rahisi katika kuyafikia mafanikio.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Rais Dkt. John Joseph Magufuli wakati akizindua rasmi wiki ya maonesho ya nne ya viwanda ikiwa ni katika kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa wakuu wa nchi 16 kutoka ukanda wa SADC, Magufuli amesema kuwa mchango wa taasisi za sekta binafsi unaonekana na wamekuwa karibu sana serikali katika kuhakikisha azma ya kujenga uchumi imara inafanikiwa hivyo hawana budi kulalamika pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali kwani hakuna njia rahisi ya kuyafikia maendeleo.
Rais Magufuli amezipongeza taasisi za sekta binafsi kwa kushiriki katika mkakati wa kujenga viwanda vipya ambapo kwa miaka mitatu pekee ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano jumla ya viwanda vipya 4000 vimeanzishwa.
"Mchango wenu ni mkubwa na unaonekana, tudumishe umoja na mshikamano kupitia jumuiya yetu katika kuhakikisha nchi wanachama zinanufaika kupitia umoja huulu ili tufike mbali zaidi mbali na kuwa na uchumi wetu wenyewe ulio imara zaidi" Ameeleza Rais Magufuli.
Kwa upande wake mwenyekiti wa taasisi za sekta binafsi nchini Salum Shamte ambaye pia leo amekabidhiwa kiti Cha uenyekiti wa baraza la biashara (SADC) kutoka kwa Bi. Charity Mwiya (Namibia) amesema kuwa kazi kubwa wanayoifanya ni pamoja na kushirikiana na serikali katika kujenga uchumi na kutengeneza ajira na wamekuwa wakishirikisha na nchi wanachama wa SADC katika masuala ya biashara kwa kuhusisha nchi wanachama.
Shamte amesema kuwa mchango wa jumuiya hiyo ni mkubwa na katika maonesho ya nne ya wiki ya viwanda watanzania wajitokeza na kutumia fursa katika kujipatia masoko, kubadilishana ujuzi na uzoefu pamoja na kutangaza bidhaa zao kwa wageni.
"Mkutano huu kufanyika hapa nchini lazima ulete mabadiliko kwa sisi wenyeji, tujitokeze kwa wingi na kunadi bidhaa zetu ambazo bila shaka zitapata soko la uhakika na hatimaye kuweza kufikia malengo ambayo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. Magufuli umedhamiria kuyafikia" Ameeleza Shamte.
Ni wazi kwamba mchango wa taasisi za sekta binafsi unachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi wa nchi mbalimbali hasa za ukanda wa SADC na nafasi ya uenyekiti iliyokabidhiwa leo kwa Salum Shamte ni daraja wezeshi zaidi katika kufikia malengo ya kujenga uchumi wa kati na kujenga taifa la viwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia makabidhiano ya Baraza la Biasha la SADC,ambapo Mh. Salum Shamte ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la SADC kutoka kwa Charit Mwiya Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la SADC aliyemaliza muda wake,katika ufunguzi wa maonesho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Agosti 5, 2019 kulia ni



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...