NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadfi VETA,
imeendelea kuja na ubunifu katika kutengeneza mashine na vifaa mbalimbakli ili
kurahisisha utendaji kazi katika maisha ya kila siku katIka jamii.
VETA ambao wako kwenye maonesho ya Nanenane
kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi Mkoani
Simiyu, banda lao limekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wanaotembeela maonesho
hayo ambapo, miongoni mwa vifaa vilivyobuniwa ni kibao cha kufulia nguo, ambapo
wanafunzi wa VETA mjini Songea kwa kushirikiana na Ruta Kamoto kutoka Shirika la
JICA. Wamebuni njian rahisi ya kufua nguo kwa kutumia kibao.
Ruta Kamoto ambaye pia ni Afisa Maendeleo
Songea vijijini alisema, kibao hicho kilibuniwa na wanafunzi wa VETA Songea ili
kumrahisishia mfuaji w anguo badala ya kutumia nguvu nyingi katika kufikicha
nguo, kibao hicho hakihitaji mayumiazi makubwa ya nguvuy katika kufua kwani ni
rahisi na hutumia mufa mfupi kufua nguo.
“Kibao hiki kina migongo midogo, unaweza
kutumia sabuni ya kipande na kupaka katika nguo kama kawaida, au kuweka nguo
katika machanganyiko wa maji na sabuni ya unga baada ya kukolea, unachukua nguo
na kuilaza kwenye kibao na kusugua taratibubu na baada ya muda mfupi nguo
itakuwa imetakata.” Alisema Ruta Kamoto.
Aidha wananchi wanaotembelea banda hilo la VETA
pia wamepata fursa ya kujionea mashine ya kusaga nyasi kwa ajili ya malisho ya
mifugo, kama vile Mbuzi na Ng’ombe ambapo mashine hiyo inaweza kutumia umeme au
jenereta.
Mbunifu Fredrick Uliki ambaye ni Mwalimu wa ufundi
mitambo VETA Morogoro, yeye alisema wao wamebuni mashine ya kukatakata malisho
ya mifugo ili yaweze kuliwa kwa urahisi, “majani yakiwa makubwa makubwa huliwa
kwa asilimia kama 30 lakini ukikata nyasi kuwa ndogondogo mnyama anaweza kula
hadi asilimia 90 ya chakula ulichompa, pia mashine inaweza kuchakata mahindi,
dagaa na mashudu ya alizeti ili kuwezesha mifugo kama ndege na kuku kula kwa
urahisi” Alifafanua Bw. Uliki.
Maonesho ya Nanenane Nyakabindi yalizinduliwa
rasmi Agosti 1, 2019 na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na yanatarajiwa
kufikia kilele Agosti 8, 2019 huku yakiwa yamebeba kaulimbiu isemayo “Kilimoi,
Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uc humi w aNchi.”.
Ruta Kamoto kutoka Shirika la
JICA akielezea jinsi kibao kinavyoweza kurahisisha kazi ya ufuaji nguo kwa wananachi waliotembela banda la VETA kwenye maonesho ya Nanenane ,kitaifa viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Mwananchi akijaribu yeye mwenyewe kufua kwa kutum ia kibao hicho ambapo alikiri kuwa ni rahisi mno.
Wananchi wakipata elimu kutoka maafisa wa VETA.

Wananchi wakipata elimu kutoka maafisa wa VETA.
Mwanafunzi wa VETA, akielezea jinsi mashine waliyobuni inavyoweza kunyoosha matairi ya gari (Wheel balance).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...