Na Woinde Shizza Michuzi TV ,Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameagiza kufungwa kamera za usalama (CCTV )katika vituo maalumu vya ukaguzi wa magari ya kusafirisha watalii ili kudhibiti matukio ya rushwa kwa askari wa usalama barabarani yanayoweza kujitokeza wakati wa ukaguzi.

Gambo ameeleza hayo leo wakati anazungumza na askari wa Jeshi la Polisi Mkoani wa Arusha, wakiwemo wa usalama barabarani katika hafla ya kutunuku motisha kwa askari waliofanikisha kukamata madini yaliyokuwa yakitoroshwa katika mpaka wa Namanga.

Amesema kuwa vituo hivyo ambavyo vimewekwa katika maeneo ya Kikatiti,Engikareti, Makuyuni na Karatu vimeanzishwa maalumu kwa ajili ya kukagua magari yanayosafirisha watalii ,ukaguzi wa vileo kwa madereva pamoja na usalama wa magari .

Amesema kuwa kufungwa kwa kamera hizo kwenye vituo vya ukaguzi wa vituo vya utalii ,kutasaidia kuondoa utata kwa baadhi ya matukio yakiwemo ya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa askari wa usalama barabarani.

"Msimamo wa mkoa ni kuhakikisha watalii wetu hawabughudhiwi na trafiki kwani wanachangia kipato kikubwa kwa Mkoa wa Arusha ambapo mkoa wetu unachangia asilimia 86 ya pato la Taifa,"amesema Gambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...