Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
Watanzania wametakiwa kula Rangi tano za mbogamboga ,matunda na viungo kwani vitu hivi vinasaidia kwa kiasi kikubwa kujikinga na maradhi mbalimbali yanayoshambulia binadamu.
Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa lishe kutoka taasisi ya kilimo cha mbogamboga na matunda (TAHA) Evarsta kimario,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ya maonesho ya nanenane yanayofanyika Ndani ya viwanja vya Themi vilivyopo Njiro jijini hapa ambapo alifafanua kuwa Rangi tano za Mbogamboga zinafaida nyingi sana katika mwili wa binadamu
Alieleza kuwa watanzania wengi wamekuwa hawana tabia wala mazoea ya kutumia matunda ya Rangi hizi tano kitu ambacho Kinasababisha hatari kubwa ya kupata magonjwa mbalimbali kama vile kisukari na presha.
"Kila tunda au mboga inafaida yake mwilini na Faida za ulaji wa Rangi tano za mbogamboga nikitoa mfano ,matunda , mbogamboga na viungo vyenye Rangi nyeupe au kahawia hizi zinakemikali za asili zinazoitwa flovonoids, Fructans ,allyl sulphides na allicim na hivi vingi vinapatikana kwa wingi kwenye kitunguu Swaumu ,kemikali hizi huinarisha Afya ya mifupa ,mzunguko wa damu mwilini,hususa ni mfumo wa umengenyaji chakula huondoa sumu mwilini na hupambana na virusi ,bakiteri na fangasi na hii huepusha miili yetu isipate magonjwa ya moyo na saratani" alisema Kimario
Aliwataka watanzania kujenga mzoea ya kula mbogamboga na matunda angalau moja katika kila mlo ambao wanaula kwakufanya hivi kutawasaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama kisukari ,kansa,tezi dume ,pia alibainisha kuwa ulaji wa vitu hivi unasaidia pia kuimarisha mifupa,kuongeza king a mwilini pia inasaidia kuimarisha ngozi isizeeke mapema
Kwa upande wake Meneja masoko wa Taha Wilibarti Mdete alisema kuwa aliwataka wananchi hususa ni wakulima kutembelea banda lao la Taha lililopo katika viwanja vya nanenane Themi Njiro kupata Elimu zaidi kuhusiana na Kilimo cha mbogamboga pamoja na matunda kwani ni kizuri na kinanufaisha wengi.
Alisema kuwa ndio msingi wa maisha ya binadamu na kwa Mtanzania, tunaambiwa daima kwamba kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi, kikiwa kinachangia asilimia kubwa ya pato la taifa na pia kilimo ni mwajiri kwa takribani asilimia 70 ya Watanzania.
Aidha aliwataka Wakulima nchini Tanzania kulima kilimo cha biashara kwa mfumo wa kilimo hai ambapo mbolea na dawa za kunyunyizia zitumike za asili badala ya zile za kisasa ili kuondokana na lishe hatarishi kwa afya ya walaji na pia kujiongezea kipato.
Akiongelea maonyesho hayo Mwenyekiti halmashauri ya Mwanga Theresia Msuya alipotembelea maonyesho hayo alizitaka halmashauri zinazoshiriki mashindano hayo pamoja na Taso kanda ya kaskazini kutumia nguvu kubwa kuyatangaza maonyesho hayo pamoja na kuwahamasisha wakulima na watanzania kutembembelea maonyesho haya na kujionea na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu kilimo na biashara.
Aidha Aliwataka wakulima kutenga bajeti yakuandaa maonyesho haya ya nane nane,ili yaboreke zaidi na wakulima waweze kujifunza zaidi mbinu mbalimbali za kilimo cha kisasa.
Maonesho haya ya nane nane ni 26 ambapo kwa kanda ya kaskazini yanafanyika Mkoani Arusha katika viwanja vya Themi Njiro Ndani ya Jiji la Arusha na mikoa inayoshiriki kutoka kanda ya kaskazini ni Manyara,Kilimanjaro ,Tanga pamoja na mwenyeji Mkoa wa Arusha ambapo kauli mbiu ni yake inasema kilimo ,mifugo na uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.
kwanza kushoto bwana shamba wa Taha wa kwanza kushoto Magembe Sugwa akimuelekeza mmoja wa mkulima alietembelea banda lao Bjarne Laustsen (mzungu) namna Taha wanavyofanya kazi katika banda lao lililopo ndani ya maonyesho ya nanenane kwa kanda ya kaskazini ambayo yanafanyika katika viwanja vya Taso vilivyopo Njiro jijini Arusha .
Mtaalamu wa lishe kutoka taasisi ya kilimo cha mbogamboga na matunda (TAHA) Evarsta kimario akiongea na waandishi katika maonyesho ya nanenane ambayo kwa Kanda ya kaskazini yanafanyika jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...