Matapeli wanaojitambulisha kama wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kwa makosa ya kudukua taarifa za wateja wa huduma ya kifedha ya Tigo Pesa inayotolewa na kampuni hiyo ambapo wamekuwa wakiwatapeli wateja wa kampuni ya Tigo kwa kujitambulisha kama wafanyakazi halali wa Tigo wakati kiukweli sio waajiriwa wa Tigo.

 Matapeli hao utumia mbinu hiyo kujipatia taarifa za siri za wateja hao ambazo baadae wamezitumia kuiba kiasi cha fedha zipatazo shilingi milioni 26 kutoka kwa wateja mbalimbali wa mtandao huo kupitia huduma ya Tigo Pesa.

Hawa watu wana mbinu mbalimbali, tukitolea mfano, kuna ambao watakupigia wakisema aidha wamekutumia hela kimakosa, au anakupigia kutoka makao makuu ya kampuni ya simu husika na angependa utatue tatizo ambalo mteja amelalamikia.

Tulipata nafasi ya kumuhoji wakala mmoja, kwa jina la Amos Chirwa kutoka Kijichi, ambae alisema, " kwa kweli matapeli ni wengi, na kila siku wanabuni njia tofauti tofauti ili waweze kutuibia sisi mawakala au wateja".

"Mimi kama wakala, ambae nina uzoefu wa miaka 6 sasa, ningependa kuwashauri watanzania kwa ujumla, kwamba usimpe mtu namba yako ya siri, au taarifa binafsi hata kama amejitambulisha kama mfanyakazi wa kampuni za simu kama Vodacom, Airtel, Tigo au Zantel". Alimalizia kwa kusema.

Mtandao huu ungependa pia kuwaasa watanzania kutojishirikisha na masuala ya kiuhalifu hususan katika masuala ya simu za mkononi kwani serikali ina mkono mrefu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...