Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Eribariki Kingu, akihutubia Wananchi wa Kijiji cha Mpetu katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Eribariki Kingu, akiwa na viongozi wa Kata ya Muhintiri mbele ya gari lenye mtambo wa kuchimba maji katika Kijiji cha Mpetu. Maji yaliyopatikana katika kijiji hicho yatakuwa yanatoka lita 11,000 kwa saa.
Mkutano ukiendelea
Mkutano ukiendelea.
Mchungaji Josephat Michael wa Kanisa la Pentecoste F.P.C.T. la Kijiji cha Mpetu akiuombea mkutano huo.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Muhintiri, Bahati Mkungile akiwatambulisha wataalamu waliopo katika kata hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzì (CCM) wa kata hiyo, Maliko Deu, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpetu, Yona Hongoa akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Muhintiri, Peter Lyimo akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wana CCM wa Kijiji cha Mpetu wakiwa wamembeba, Shabani Ramadhani aliyehamia chama hicho kutoka Chadema.
Jonatha Nkhundi aliyehamia CCM kutoka Chadema akizungumza.
Wanakwaya ya Huruma ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Muhintiri wakitoa burudani.




Na Dotto Mwaibale, Singida

WANANCHI wa Kijiji cha Mpetu Kata ya Muhintiri wilayani Ikungi mkoani Singida wamempongeza Mbunge wao wa Singida Magharibi, Eribariki Kingu kwa kazi kubwa ya maendeleo anayoifanya katika jimbo hilo kwa kushirikiana na Serikali.

Hayo yalibainishwa jana na mkazi wa kijiji hicho, Yona Hongoa katika mkutano wa hadhara aliouandaa mbunge huyo kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuwahamasisha 

kujitokeza kwa wingi kujiandika katika daftari la kudumu la mpiga kura na kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapata ushindi kwenye chaguzi zake kuanzia wa viongozi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu.

"Kwa kweli tunampongeza mbunge wetu kwa kazi kubwa anayoifanya katika jimbo letu kwani tangu kijiji chetu kianzishwe hatukuwahi kuwa na maji lakini amefanikisha kutuletea ikiwemo ujenzi wa shule, Zahanati pamoja na barabara" alisema Hongoa.

Diwani wa Kata ya Muhintiri, Peter Lyimo akizungumza katika mkutano huo alisema katika utekelezaji wa ilani ya CCM, Mbunge huyo ameweza kuchangia fedha nyingi kutoka mfukoni mwake na mfuko wa jimbo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

" Kwa kazi hii kubwa anayoifanya mbunge hatuna wasiwasi CCM itapata ushindi wa kishindo ambao haujawahi kupatikana katika uchaguzi wowote tuliowahi kuufanya" alisema Lyimo.

Akizungumza katika mkutano huo Kingu aliwashukuru wananchi na kuwaambia maendeleo hayo wanayapata baada ya Rais John Magufuli kuwabana mafisadi na matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kuzielekeza kwa wananchi kwa kuwapelekea miradi ya maendeleo.

Alisema haijawahi kutokea kwa kipindi chote kilicho pita ndani ya jimbo hilo kufanyika kwa miradi mingi kiasi hicho ikiwemo miradi mikubwa ya maji na kuwa kazi hiyo inaendelea jimboni humo.

Kingu alisema kuna zaidi ya sh.milioni 300 zimeelekezwa kutekeleza mradi wa maji katika kijiji hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...