Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa akizungumza na Vijana wa Mkoa wa Ruvuma kuhusu Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo katika Mkoa wa Ruvuma, Agosti 10, 2019.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Hakimu Mafuru akizungumza na vijana walioshiriki katika mafunzo hayo ya ujasiriamali yaliyofanyika katika mkoa huo. (Kulia) ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Bw. Philliph Beno.
Baadhi ya vijana wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi wakifuatilia maelezo ya Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa (hayupo pichani) alipokuwa akielezea kuhusu Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali.
Sehemu ya wajasiriamali wanaomiliki biashara wakifuatailia maelezo ya Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo hayo katika mkoa huo.
Meneja wa Ufuatiliaji na Tathmini Bi. Flora Kajela akielezea kuhusu malengo ya Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Mkoa wa Ruvuma.
Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Daudi Sailasi akielezea kuhusu programu ya kuongeza ujuzi kwa vijana inayoratibiwa na ofisi hiyo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara yaliyofanyika katika Mkoa huo. (Kulia) ni Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa.
Mwezeshaji kutoka Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bw. Lucas Mafuru akitoa mada kuhusu uchambuzi wa ushindani na mikakati ya masoko kwa wajasiriamali (hawapo pichani).
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eliakim Mtawa akitoa mada kuhusu vihatarishi vya biashara na namna ya kuvikabili kwa wajasiriamali walioshiriki mafunzo hayo.
Mmoja wa Wajasiriamali Bw. Richard Mpagala akielezea kuhusu mbinu anazotumia kuendesha biashara yake alipokua amejifunza kuhusu masuala ya mapato na matumizi katika usimamizi wa biashara.
Bi. Pudencia Msangawale akionesha bidhaa anazotengeza na akielezea mbinu anazotumia kutafuta masoko ya bidhaa zake katika eneo lake la biashara.
Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo ya Ujasiriliamali kutoka kwenye Ofisi hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi za Umma.
Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajasiriamali walioshiriki mafunzo hayo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara.

……………………………………………………..

Vijana Mkoa wa Ruvuma wamefurahia fursa ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamaizi wa biashara yaliyotolewa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo yatawawezesha vijana hao kukuza na kurasimisha shughuli zao za kiuchumi.

Akifungua Mafunzo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’I Issa alieleza kuwa mafunzo hayo ya ujasiriamali ni muhimu sana na yanalenga kuwawezesha vijana wanaomiliki biashara wanapata mbinu za kuendeshaji na kusimamia biashara zao.

“Mafunzo haya ya ujasiriamali yameleta tija kwa vijana na wameweza kujiajiri kwa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi zenye faida,” alisema Issa

Alieleza kuwa vijana wanapaswa kuchangamkia fursa hizo zinapojitokeza ili waweze kuunganishwa na fursa za mitaji na mitandao ya huduma za biashara, pia kuwajengea uwezo wa kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa kujiamini na kuweza kuweza kupata faida.

“Vijana mnapaswa kutambua ninyi ndio nguvukazi ya Taifa, hivyo kuwa wabunifu ni jambo la msingi katika biashara zenu mkitambua fursa mlizonazo ili muweze kushindana katika biashara,” alisema Issa

Akibainisha aina ya mafunzo ya ujasiriamali watakayopatiwa vijana hao yakiwemo masuala ya uchambuzi wa masoko, dhana ya ujasiriamali, uchambuzi wa mahitaji ya mteja, kutambua ushindani wa soko, mkakati na uendeshaji biashara, utambuzi wa masoko, usimamizi wa fedha, vihatarishi vya biashara na namna ya kuvikabili, usimamizi wa biashara na rasilimali watu, urasimishaji wa biashara na vyanzo vya mitaji.

Aliongeza kuwa Programu hii ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana itawawezesha kutambua mapungufu waliyonayo na kutumia mwanya huo kuangalia fursa walizo nazo katika ushindani wa biashara zao.

“Ni muhimu vijana mkawekeza katika biashara mnazozimudu kimtaji, kiusimamizi kwa ushindani na kufanya maamuzi sahii,” alieleza Issa

Alieleza kuwa kila Mkoa una fursa zinazoweza kutumiwa na wajasiriamali katika kujiendeleza kiuchumi, vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa hizo ili waweze kunufaika kwa njia mbalimbali.

Alifafanua kuwa Ofisi yake imekuwa ikiendesha mafunzo ya aina hii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Taasisi za Umma, Wadau wa Mendeleo, Sekta binafsi na jamii kwa ujumla.

“Zaidi ya Vijana 10,000 wameweza kufikiwa na programu mbalimbali za mafunzo ikiwemo Kijana jiajiri, Ajira yangu, Kliniki ya vijana wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu, mifuko ya uwezeshaji na watoa huduma,” alisema Issa

Aidha, alitoa shukrani zake kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuona haja ya kuwekeza kwa vijana kwa kuwapatia ujuzi ili waweze kujiajiri, kuajiri na kuchangia katika pato la taifa.

Kwa Upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Hakimu Mafuru amewahimiza vijana wa Mkoa huo kuchangamkia fursa za mafunzo kama hayo yanayotolewa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali kwa kuwa yatawawezesha kujitambua na kujisimamia wenyewe na kuongeza tija kwenye biashara zao.

Mmoja wa Vijana walioshiriki katika Mafunzo hayo, Bi. Pudencia Msangawale alieleza kuwa mafunzo hayo yatajibu changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kama wajisiriamali ikiwemo masuala ya ujuzi, maarifa, kurasimisha biashara, namna bora ya kuhudumia wateja na utafutaji wa masoko.

“Ninawashukuru Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa elimu waliyotupatia yametuwezesha kujitambua, kuwa wabunifu, waaminifu na kuweza kujisimamia katika biashara,” alisema Msangawale.

Mafunzo hayo yanaratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo yatafanyika katika Mikoa nane (8) ya Tanzania Bara ikiwemo Dodoma ambapo tayari yamekisha fanyika, Ruvuma, Geita, Mwanza, Lindi, Mbeya, Tanga na Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...