Viongozi hususani
wa Serikali kuanzia ngazi ya Kijiji wametakiwa kuchukua hatua ili kupambana na utoro
kwa wanafunzi katika Shule mbalimbali za Msingi na Sekondari zilizopo Wilaya
Tarime mkoani Mara unaochangia kudhorotesha kiwango cha elimu.
Rai hiyo
ilitolewa jana Agosti 05, 2019 kwenye mdahalo wa utoaji elimu ya kupambana na
vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi
hususani wa kike uliofanyika katika Kata ya Muriba wilayani humo.
Mdahalo huo
ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo mpango mkakati wa kitaifa wa kupambana na aina
zote za ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA) ambapo Wilaya
Tarime inatekeleza mpango huo kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za
wanawake na wasichana (KIVULINI).Na George Binagi-GB Pazzo, Tarime
Taswira ilivyokuwa kwenye kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Kata ya Muriba wilayani Tarime.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akitoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo kuachana na mila ya ukeketaji kwenye mdahalo huo.
Afisa Elimu Kata ya Muriba wilayani Tarime, Mwl. Kefa Odao akitoa rai kwa wazazi na walezi katika Kata hiyo kuacha kuwapangia majukumu watoto wao siku za masomo hatua inayochochea ongezeko la utoro mashuleni.
Viongozi na watendaji mbalimbali wilayani Tarime wakifuatilia mdahalo huo.
Waendesha bodaboda katika Kata ya Muriba wilayani Tarime waliunga mkono juhudi ya kupambana na ukatili wa kijinsia hususani kupambana na mimba na ndoa kwa wanafunzi.
Wanaharakati wa kujitolea waliopewa mafunzo na shirika la KIVULINI kusaidia utoaji elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia ngazi ya jamii wakiongoza maandamano ya kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu kupinga aina zote za ukatili katika jamii.
Wanaharakati wa kujitolea wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kupinga aina zote za vitendo vya ukatili katika jamii.
Wanafunzi wakitoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia kwa njia ya nyimbo.
Tazama Video hapa chini


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...