Na Woinde Shizza,Michuzi Tv,Arusha

Watanzania wametakiwa kuwatunza watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu na hatarishi ,kwa kuwa watoto hao wengi wao Wana ndugu hapa nchini lakini pia baadhi  ya wazazi wao wapo hai.

Akizungumza katika hafla ya kufungua kituo cha Amani Cha Makazi Salama na kuokoa watoto wa mitaani kilichopo kaloloni Jijini Arusha, Kamishna wa Ustawi wa Jamii,Dkt.Naftali Ng'ondi amesema kuwa dhana ya kuliacha kundi hili kutunzwa tu na wageni kutoka nje ya nchi haileti taswira nzuri.

Aidha Dkt.Ng'ondi alisema kuwa ni vyema watanzania wakajenga utaratibu wa kuchangia Kundi hili ili kupunguza baadhi ya changamoto badala ya kuwaachia wageni kutoka nje.

"Hii dhana haileti taswira nzuri Jamani tumekuwa tukiwaachia wageni tu kuchangia kuanzia masomo , chakula,na mengineyo kwanini hatujishughulishi na hawa watoto wakati ni watanzania "alihoji dkt.Ng'ondi

Hata hivyo aliitaka kamati ya ulinzi kwa watoto mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa inaendelea kutoa elimu Juu ya ukatili kwa mtoto kwa kuwa takwimu zinaonesha kuwa vitendo hivyo vimekidhiri katika mkoa wa Arusha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Amani na Makazi Salama Cha kuokoa watoto wa mitaani Mendert Schaap alisema kuwa kituo hicho kinalea watoto zaidi ya 300 na kuwapatia elimu na kuwakutanisha na wazazi wao.

Bw.Schaap alisema kuwa mbali na kuwawezesha watoto wanaoishi mitanii makazi hayo Salama,yatawawezesha watoto kupatiea misaada Mbali Mbali na kujiendekeza kiuchumi na kielimu.

Mmoja wa watoto aliyeokolewa mtaani anayefahamika kwa jina la Marry Christopher (19) alisema kuwa aliingia mtaani akiwa na miaka kumi tu na aliweza kuishi ndani ya miaka miwili mtaani Kama mtoto wa kiume ili aweze kukwepa vitendo vya ukatili.

Marry alisema kuwa kituo cha Amani kimeweza kumpatia elimu na Sasa ni mwalimu ambaye anafundisha kuchomelea vitu Mbali Mbali na kuwataka watoto wa mitaani pindi wanapokolewa kutumia vyema nafasi ya elimu na kupata ujuzi .
kamishina wa Ustawi wa Jamii,Dkt.Naftali Ng'ondi akikata utepe ishara ya ufunguzi rasmi Wa kufungua kituo cha Amani Cha Makazi Salama na kuokoa watoto wa mitaani kilichopo kaloloni Jijini Arusha

 kamishina wa Ustawi wa Jamii,Dkt.Naftali Ng'ondi  akiongea na waandishi Mara baada ya kituo hicho kufunguliwa
Mkurugenzi wa kituo cha Amani na  Makazi Salama Cha kuokoa watoto wa mitaani  Mendert Schaap akiongea na waandishi Mara baada ya kituo hicho kufunguliwa
Baadhi ya wafadhili kutoka nje waliochangia ujenzi huo Wa kituo cha watoto cha Amani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...