Waziri Mkuu ameishukuru Tigo kwa kuwa mdhamini rasmi wa intaneti itakayotumiwa na wageni wanaohudhuria mkutano wa 39 wa jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea banda la Tigo na kuwapongeza kwa kuwa wadhamini rasmi wa intaneti itakayotumika kwenye mkutano wa 39 wa jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC ) unaondelea jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere. Tigo ndio kampuni ya mawasiliano pekee yenye mtandao wa kasi wa 4G+.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikaribishwa na Mkuu wa Mauzo – Tigo Business, Kadambara Maita katika banda la Tigo, lililopo katika mkutano wa 39 wa jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC unaondelea jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.


Wafanyakazi wa Tigo wakimkaribisha Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa, katika banda la Tigo, lililopo katika mkutano wa 39 wa jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC unaondelea jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...