Na Said Mwishehe,Michuzi TV 

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imetaja maeneo matatu ya kimkakati ambayo nchi ya Tanzania itanufaika nayo kupitia mikutano inayoendelea kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC).

Akizungumza leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwlimu Nyerere jijini Dar es Salaam Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalim amesema Tanzania kupitia Mkutano wa SADC kuna mambo mengi tutanufaika nayo.

Waziri Mwalim ametaja baadhi ya maeneo ambayo nchi yetu itanufaika ni pamoja na MSD  kutoa huduma za dharura kwa washiriki wa mkutano wa SADC 

Akifafanua zaidi Waziri Mwalim baada ya kutembelea mabanda ya Afya  yakiwemo ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya  Moyo ya Jakaya Kikwete ma Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) amesema sekta ya afya imejipanga katika maeneo makubwa matatu.

"Maeneo hayo ni pamoja na kutoa huduma ya dharura na kusisitiza kuna vyumba vimetengwa kwa ya kutoa huduma ya matibabu kwa mtu atakayekuwa na tatizo ya kiafya,"amesema.

“Pia kwa kutumia maonesho hayo sekta ya afya nchini inaonesha uwezo, ubunifu na utashi wa kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya utalii wa kimatibabu na kupitia hospitali ya Taifa ya Muhimbili  wamepandikiza vifaa vya kusikia kwa watoto na kutibu kwa kutumia radioloji,"amesema.

Waziri Mwalim amesema  huduma hizo zilikuwa hazipatikani nchini wala kwa nchi za SADC huku akitoa mfano upandikizaji wa figo ambapo ukitoa nchi ya Afrika Kusini nchi nyingi hazijaanza  kutoa huduma za kupandikiza figo.

Wakati huo amesema mkutano wa SADC wataeleza na kuwaonesha washiriki wa mkutano huo ni kwa namna gani Tanzania ambavyo imepiga hatua kwa kutoa huduma za kibingwa.

"Kwa mazingira hayo nchi za SADC hazina haja ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi za jumuiya hiyo.Wagonjwa waletwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH).Kila mwezi inapokea wagonjwa 24 kutoka nchi za SADC  na hasa nchi za Comoro,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Malawi.

Amesema Wizara ya Afya inaamini mkutano wa SADC utaongeza idadi ya wagonjwa kuja nchini Tanzania kwa ajili ya matibabu." Muhimbili kwa mwaka tunapokea wagonjwa  284 kwa nchi za SADC,"amesema.

Pia amesema eneo la tatu  ni utoaji wa zabuni na kufafanua Tanzania itanufaika na ununuzi wa dawa,kwani MSD imepata  mkataba wa kusambaza dawa kwa nchi za SADC.

Amesema mawaziri wa afya wa nchi za SADC kwa umoja wao waliamua kuipa mkataba MSD  wa kununua na kusambaza dawa."Kupitia maonesho haya ya SADC yamechochea utaratibu wa kusambaza dawa na zabuni za kununua imeshakamilika,"amesema  na kuongeza nchi za Mauritius , Botswana na Lesotho zimekubali kununua dawa kupitia utaratibu wa nchi za SADC. 
 Wataalam wa afya wa Muhimbili, MOI, JKCI na Hospitali ya Lugalo wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mh.Ummy  Mwalimu katika viwanja vya ukumbi  wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC). 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto  Mh.Ummy Mwalimu akisoma jarida la Muhimbili linaloeleza huduma mbalimbali za afya zinazopatikana MNH. Kulia ni Dkt. Juma Mfinanga akimweleza jambo Waziri. 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mh.Ummy Mwalimu akimuonesha jambo Dkt. Juma Mfinanga 
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Mafunzo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Pedro Pallangyo akimweleza v huduma zinazopatikana JKCI zikiwamo huduma za tiba ya umeme wa moyo na  kuzibua mishipa ya damu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...