Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mwenyekiti wetu Dk Mshindo Msolla amesema awamu ya tatu ya shehena ya jezi za Yanga inatarajiwa kuwasili wakati wowote ambapo kutakuwa na mabadiliko ya bei ya jezi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la Yanga Kaloleni jijini Arusha jana, Dk Msolla amesema kutakuwa na punguzo la bei ili kuwawezesha mashabiki na wanachama kununua kufuatana na uwezo wao.

Amesema,” Zile jezi tulizozindua kwenye awamu ya kwanza zilikuwa toleo daraja la juu ambazo zilikuwa za wachezaji ziliuzwa kwa Tsh 35,000/- na baadae likaletwa toleo la mashabiki ambazo ziliuzwa Tsh 30,000/-".

Ameeleza kuwa wamefanya mazungumzo na GSM na kukubaliana kuwa jezi za awamu ijayo, lile toleo la juu zitauzwa kwa Tsh 30,000/- na zile za mashabiki zitauzwa Tsh 20,000/-.

Msolla amesema Lengo kuu ni kuwawezesha mashabiki na wanachama wa Yanga kununua jezi original kulingana na uwezo wa kila mmoja na kuiongezea timu mapato.

Aidha Dk Msolla amesema ujio wa jezi hizo utamaliza changamoto ya kukosekana kwa jezi mpya za Yanga madukani,Kampuni ya GSM imeahidi kuwezesha upatikanaji wa jezi za Yanga nchi nzima na bei elekezi.
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt Mshindo Msolla akizungumza na wanachama wa Yanga mara baada ya kuzindua tawi la Kaloleni Arusha na kuelezea mabadiliko ya bei ya jezi hizo kwa awamu ya tatu pindi itakapoingia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...