WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) Agosti 26 mwaka 2019.

Akizungumza leo Agosti 19,2019 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho Shekha Nasser amesema sekta ya urembo na vipodozi inakua kwa kasi na kutoa ajira nyingi kwa watanzania walio wengi.

"Tukio hilo la kihistoria la kuzindua chombo hiki muhimu ndani ya nchi yetu litafanyika Agosti 26, 2019 katika jengo la PSSSF –KISENGA, Kijitonyama . Mgeni rasmi ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,"amesema.

Amefafanua wamekuwa wakishuhudia ongezeko la warembaji, wenye salons, watengeneza kucha, watengenezaji na wanaoingiza bidhaa za urembo na vipodozi,hivyo ni wakati muafaka kuwa na chama chao ambacho kitaaunganisha wadau wote.

Amesisitiza TCA ni chama kinachoanzishwa mahsusi kwa ajili ya kuhudumia na kuunganisha wadau wote katika sekta ya urembo na vipodozi nchini."Chama hiki kitahusisha wadau wote kuanzia waelimishaji, wajasiriamali wakubwa na wadogo, wazalishaji wa viwanda vidogo na vikubwa.

"Pia watengenezaji wa bidhaa asilia, watoa huduma, wasambazaji na watabibu wa ngozi katika sekta nzima hii ya urembo na vipodozi,"amesema.
Amesema kupitia ndani ya ya TCA kutakua na mafanikio ya kukuza sekta ya urembo na vipodozi baada ya kuona changamoto nyingi wanazozipitia washikadau.

Ametoa mfano pamoja na Wizara ya Elimu kupitia NACTE kupitisha mtaala wa kwanza wa elimu ya Stashahada hivi karibuni, lakini vyuo vya kutoa NTA Level 4, 5 na 6 bado havipo. 

Ameongeza pamoja na VETA kuwa na mtaaala wa kozi ya cheti cha Cosmetology lakini changamoto kubwa ni walimu wenye sifa ya Diploma wa kufundisha wanafunzi ili wafanye mtihani wa Taifa na kupata walimu wenye Weledi na sifa nchini. 

Amesema kuwa ukosefu huo wa walimu wa Cosmetology nchini unasababishwa na mambo mengi yakiwemo ya sekta hiyo kutotambulika rasmi na kujengewa heshima yake inayostahili kama ilivyo katika nchi za jirani Kenya, Uganda na South Afrika.

"Watanzania wengi huenda kwenye nchi hizo kwa ajili ya kujifunza na kupata elimu ya Cosmetology ngazi ya Stashahada,"amesema Nasser na kuongeza kutokana na muamko huo wameona ni wakati muafaka wa kuanzisha chombo kitakachowaunganisha wadau wote wa sekta hiyo.

Mwenyekiti huyo wa TCA ametumia fyrsa hiyo kuwakaribisha wadau wote wa sekta ya urembo nchini Tanzania kufika ili kushuhudia tukio hilo la kipekee kwa mara ya kwanza Tanzania lenye kauli mbiu " Urembo na vipodozi katika uchumi wa Viwanda". 

 Mwenyekiti wa Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) ,Shekha Nasser  akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar kuhusu  uzinduzi  wa chama hicho, Agosti 26,mwaka 2019, ambapo Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.Kulia ni Katibu wa TCA Braison Makena na kushoto ni Meneja Utawala TCA,Judy Charles  
Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...