Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amesema kuwa hivi karibuni Bunge hilo kuacha kutumia mfumo unaotumika sasa wa kuwapa Wabunge nyaraka mbalimbali, kwa kuhamia katika mfumo wa Digitali wa kuwawekea nyaraka hizo kupitia simu zao za mikononi.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo Bungeni jijini Dodoma, wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge la 11, ambapo amesema katika Afrika Mashariki, Tanzania pekee ndiyo ambayo Bunge lake bado linatumia mfumo wa karatasi.

Spika Ndugai amesema kuwa "sisi ndiyo Bunge pekee Afrika Mashariki ambao tunaendekeza Makaratasi mengi, wenzetu hawatumii, tunaanza na hii 'Order Paper' halafu tutaenda kidogo kidogo"

"Mpaka tufike hatua dawati la Mbunge liwe safi, naombeni mhakiki simu zenu na barua pepe, tunaanza kuwapatia nyaraka." ameongeza Spika Ndugai.
Leo Septemba 03, 2019 mkutano wa Bunge la 16 umeanza jijini Dodoma, ambapo Miraji Mtaturu aliapishwa kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, akirithi nafasi ya Tundu Lissu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...