Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Kitengo cha Afya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, kimeendesha zoezi la utayari kukabiliana na magonjwa mlipuko hususan Ebola ambayo imeendelea kushambulia nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda.

Zoezi hilo la utayari linafanyika kutokana na Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Kitovu cha Biashara kwa Taifa kwa Wageni wengi kufika kwa ajili ya Biashara hizo. Mikoa Tisa nchini iliyo jirani na nchi hatarishi, imetajwa kuwa kunyemelewa na ugonjwa huo.

Akizungumza na Michuzi TV, Michuzi Blog wakati wa zoezi hilo lililofanyika katika Hospitali za Amana na Temeke, Mtaalamu wa Udhibiti wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Dkt. Elibariki Mwakapeje amesema zoezi hilo limefanyika katika mkoa wa Dar es Salaam kutokana na tishio nchi za jirani.

Dkt. Mwakapeje amewapongeza Dar es Salaam kujiandaa vizuri katika zoezi hilo kwa kuandaa mazingira yakukabiliana na ugongwa huo katika maeneo ya vituo vya afya, ametoa wito kwa mikoa mingine nchini kufanya zoezi hilo ili kupima utayari wao katika kupambana na ugonjwa wa Ebola na magonjwa mlipuko.

Mratibu wa Huduma za Dharura na Maafa, Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Christopher Mzava amesema Mkoa wa Dar umetoa mafunzo mbalimbali kwa wiki nzima kwa Watumishi wa Afya katika Halmashauri Tano ili wapate uelewa kuhusu ugonjwa huo, amesema elimu inaendelea kutolewa namna yakumfahamu mgonjwa na kuzuia ugonjwa wa Ebola.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Yunus Ngungile amewatoa hofu Wananchi wa Mkoa huo, amesema Serikali inaimarisha mifumo ya ufuatiliaji ili kujikinga kwa wakati dhidi ya Ugonjwa huo, amesema mapungufu yaliyoonekana katika zoezi hilo yatafanyiwa kazi kuyaboresha na kuimarisha kwa kutoa huduma bora kwa Wagonjwa waliokumbwa na gonjwa hilo Ebola.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Amana, Dkt. Amani Malima amesema wamewapa mafunzo Watumishi wao na Watu wote wamepewa tahadhari ya ugonjwa huo, amesema vifaa kwa ajili ya kujinga vimeandaliwa, pia kutenga maeneo maalum endapo kuna viashiria vya ugonjwa huo, amethibitisha Hospitali ya Amana hakuna Mgonjwa yeyote aliyegundulika kuwa na Ebola.


DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA:

Homa kali ya ghafla, Joto la mwili kupanda, Kutapika, Kutokwa na Damu sehemu zote za mwili, Kuharisha, Historia ya kufanya kazi au kutoka maeneo yaliyokumbwa na tatizo hilo. 
 Wauguzi wa Hospitali ya Temeke wakiendelea na zoezi la utayari kwa Mogonjwa wa Ebola alipofikishwa kituoni hapo kwa matibabu.
 Mmoja wa Wauguzi katika Hospitali ya Amana akimsikiliza Mgonjwa wa Ebola aliyeletwa Kituoni hapo wakati wa  zoezi la utayari kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola.
 Mgonjwa aliyekumbwa na Ebola akishushwa katika Gari maalum la kubebea Wagonjwa (Ambulance).
 Maandalizi yakiwa tayari kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola 
Mratibu wa Huduma za Dharura na Maafa, Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Christopher Mzava akizungumzia tahadhari inayotakiwa kuchuliwa dhidi ya Ugonjwa wa Ebola. 
 Mtaalamu wa Udhibiti wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Dkt. Elibariki Mwakapeje akizungumza na Michuzi TV wakati wa zoezi la utayari kupambana na magonjwa mlipuko yakiwemo Ebola.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...