Na Jusline Marco-Arusha

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga ameiagiza sekretarieti ya Mkoa wa Arusha, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya kusimamia zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa kikamilifu pamoja na kutoa ushirikiano kwa wasimamiza wa uchaguzi wa serikali za mitaa. 

Akizungumza katika zoezi la uapishwaji wa wazimamizi wa zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Septemba mwaka huu pia ameagiza migogoro iliyopo baina ya wananchi na viongozi itatuliwe na amani idumishwe katika jamii ili kuhakikisha zoezi la uchaguzi linafanyika na kumalizika vyema.

Aidha pamoja na zoezi la uapishwaji kwa watumishi hao bado walikabidhiwa na changamoto ya vifaa vya uchaguzi ambavyo ni Tangazo la uchaguzi wa serikali za mitaa, kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa, Muongozo wa uchaguzi wa serikali za mitaa na ramani ya mipaka.

Watumishi ambao wameapishwa chini ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arusha Mhe. Pendo Mushi ili kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa Mkoani Arusha ni pamoja na Msena Nyamwiling'i Bina Mkuu wa idara ya utumishi na utawala halmashauri ya Jiji la Arusha, Hussein Ramadhan Mgewa Mkuu wa idara ya elimu msingi halmashauri ya wilaya ya Arusha, Pius John Haule Mkuu wa kitengo cha uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Karatu.

Aidha watumishi wengine ni Natang’aduaki Zakayo Mollel Mkuu wa idara ya elimu msingi halmashauri ya wilaya ya Longido, Jonathan Peter Kima Mkuu wa kitengo cha sheria halmashauri ya wilaya ya Meru, Theresia Evarist Kyara, mkuu wa idara ya mipango, takwimu na ufuatiliaji halmashauri ya wilaya ya Monduli na Emmanuel Joseph Mhando Mkuu wa idara ya utawala na utumishi halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro.

Sambamba na zoezi la kuapishwa, watumishi hao walikabidhiwa vifaa vya uchaguzi ambavyo ni Tangazo la uchaguzi wa serikali za mitaa, kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa, Muongozo wa uchaguzi wa serikali za mitaa na ramani ya mipaka.
Mkuu wa idara ya Utumishi na  Halmashauri ya Jiji la Arusha,Msena Nyamwiling’i Bina, akiapishwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...