Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Edward Mpogolo amewataka wahandisi wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanatoa ushauri katika kila mradi unaojengwa kwa nguvu za wananchi.

DC Mpogolo amesema ni jambo la kushangaza kuona wananchi wanamuunga mkono Rais Dk John Magufuli kwa kushirikiana na Serikali kujenga miradi mbalimbali halafu hawapati ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wahandisi.
Hayo ameyasema wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi anayoifanya kwenye Wilaya hiyo.

DC Mpogolo amesema toka ameanza ziara hiyo na kukagua baadhi ya miradi inayojengwa kwa nguvu za wananchi vikiwemo vyumba vya madarasa hakuna sehemu yeyote ambayo wahandisi wamefika na kutoa ushauri wao.

” Hakuna mradi wenye nguvu za wananchi ambao watalaamu letu wamefika na kutoa ushauri. Hivyo nawaagiza kutoka ofisini na kuja huku kushauri kuliko Wananchi wanatumia nguvu na kidato chao halafu watumishi wanaopaswa kuwahudumia wao wamekaa tu ofisini.

” Nimepita kwenye mashule, zahanati kote huko watalaamu hawajafika, wanasubiri fedha zinazotoka juu kwa kuwa zina posho hii wanaiacha kwa kuwa haina posho, sasa natoa agizo na litekelezwe,” Amesema DC Mpogolo.

Aidha amewataka wataalamu hao kupita kwenye miradi yote iliyopo kwenye Kata za Wilaya hiyo na kumletea ripoti inayoonesha miradi waliyoitolea ushauri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...