Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango,akizungumza wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Hazina SACCOS, Aliko Mwaiteleka,akitoa taarifa wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango,akiwa katika picha ya pamoja na wanachama mara baada ya kuzindua hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.



Charles James, Michuzi TV

BENKI Kuu ya Tanzania imetakiwa kufanya utafiti wa Taasisi zote ndogo za kifedha nchini ili kuona kama kweli riba wanazoweka kwenye mikopo zina faida za msingi au zinawaumiza wanachama.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati wa uzinduzi wa ugawaji hati za viwanja vya wanachama wa Taasisi Ndogo ya Fedha ya Hazina Saccos.

Taasisi hiyo inaundwa na wanachama kutoka wizara ya fedha pamoja na watumishi wengine kutoka Serikali Kuu na Serikali za Mitaa na Taasisi zingine za Umma." Niitake Benki Kuu kufanya utafiti huo ili kubaini endapo hizo riba zilizopo kwenye mikopo ambayo wanachama wa Saccos wanapata ni rafiki au zinawaumiza.

" Nafahamu changamoto kubwa kwenye taasisi nyingi ndogo za fedha (Saccos) ni ubadhirifu niwatake viongozi wote wa Hazina na Saccos zote nchini kuwa waadilifu na kulinda maslahi ya wanachama wao," Amesema Dk Mpango.

Waziri Mpango amewataka wanachama watakaopata mikopo ya viwanda hivyo kuhakikisha wanaendeleza viwanja hivyo kwa kujenga nyumba za makazi, za kupangisha na hata majengo ya ofisi.

Ameipongeza Saccos hiyo kwa namna walivyoamua kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika kufanya uendelezaji wa Jiji la Dodoma ambalo Rais alilirasimisha kuwa Makao Makuu ya Nchi, Serikali na Chama na kuwaahidi kuwa Balozi wao katika kuitangasa Saccos hiyo.

" Nafurahi kuona hamjagawa viwanja tu mmenda mbali zaidi kwa kugawa hati kwa wanachama. Niwakumbushe Dodoma kuna fursa kubwa kila mmoja wenu azitumie kwa faida yake na Taifa kwa ujumla," Amesema Waziri Mpango.

Nae Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Aliko Mwaitegete amemshukuru Waziri Mpango kwa kukubali kuwa Balozi wao huku akimuahidi kuhakikisha wanakua Taasisi imara yenye kujali maslahi ya wanachama wake ambao wengi ni wa kada za chini.

Amesema wanahudumia watumishi zaidi ya 5000 kutoka Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Taasisi zingine za Umma." Kazi yetu ni kukusanya michango ya wanachama wetu na kuwagawia mikopo ya bei nafuu. Tayari tumeshapata viwanja 450 ambavyo tutavigawa kwa wanachama wetu muda siyo mrefu, " Amesema Mwaitegete.

Aidha amemshukuru mlezi wa Saccos hiyo ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dotto James kwa namna ambavyo amekua akijitoa kuwasimamia katika mambo mbalimbali ikiwemo ushauri wa namna gani wa kujiendesha kisasa lakini pia kwa kuwapa ofisi kwenye majengo ya Wizara ya Fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...