KATIKA kuendeleza jitihada za kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kituo cha afya cha PCMC kilichopo jijini Dar es Salaam kimetoa semina elekezi kwa wafanyakazi ili kuweza kujenga uelewa kwa jamii kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza na namna ya kukabiliana nayo pamoja na kuendesha bonanza lililoshirikisha michezo mbalimbali.

Akizungumza katika semina kwa wafanyakazi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam mkuu wa kituo cha afya cha PCMC ,  Richard Ulanga amesema kuwa semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wafanyakazi kuhusiana na uhamasishaji kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza na namna ya kuepukana nayo.

Amesema kuwa licha ya semina hiyo kutakuwa na mashindano mbalimbali na hiyo yote ni katika kuhamasisha jamii katika suala zima la kufanya mazoezi ukizingatia jiji la Dar es Salaam tatizo hilo limekuwa kubwa kutokana na mifumo ya maisha, vilevile wamewahusisha vijana wa bodaboda ambao ni sehemu ya vijana wengi wanaamini watakuwa mabalozi kwa sehemu kubwa.

Katika bonanza hilo la michezo ambalo lililenga kuhamasisha jamii umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ya kuimarisha afya, michezo kama kukimbia, mpira, kukimbia na ndimu kwenye vijiko na  kuvuta kamba ilioneshwa na makundi mbalimbali ya washiriki.

Kuhusiana na suala la kuchangia damu Ulanga amesema kuwa jambo hilo lipo kwenye mkakati kwa kuwa mahitaji ya damu ni makubwa na wakiwa Kama wadau wa afya lazima wahakikishe mahitaji ya namna hiyo yanapatikana ili waweze kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji wa damu.


Amesema kuwa kituo hicho chenye matawi Upanga, Kigamboni na Kimara kinaendelea kutoa huduma bora kupitia madaktari bingwa wa hospitali hiyo, na wamekuwa wakifanya tathimini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya pamoja na kufanya utalii katika sehemu mbalimbali.
Kiongozi Mkuu wa Kituo cha Afya cha PCMC, Richard Ulanga akitoa mafunzo kwa watumishi wa Kituo hicho wakati wa Bonanza la wafanyakazi hao yaliyofanyika katika ofisi zao zilizopo Kimara jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha Afya cha PCMC wakichangia mada kwenye mafunzo ya kuwaongezea ujuzi wakati wa bonanza lililowakutanisha watumishi hao leo jijini Dar es Salaam leo. 
 

Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye mafunzo 
Kiongozi Mkuu wa Kituo cha Afya cha PCMC, Richard Ulanga  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Bonanza la kituo hicho lililowakutanisha wafanyakazi pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi hao katika ofisi zao zilizopo Kimara jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...