Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Nelson Olotu likiwa kanisani tayari kwa Ibada ya Maziko.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika ibada ya mazishi katika kanisa la KKKT Usharika wa Sasi mtaa wa Ilmeshorori,Dayosisi ya Kaskazini Kati

Umati wawatu waliojitokeza wakiwa nje ya kanisa baada kumalizika kwa Ibada
Gari lioilobeba mwili wa Nelson likiondoka eneo la kanisa kuelekea makaburini kwaajili ya maziko.


Na.Vero Ignatus,Arusha

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati Dk.Solomon Masangwa jana ameongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Urubani Nelson Olotu (25) aliyefariki kwa ajali ya ndege Septemba 23 mwaka huu, huko Seronera Serengeti Mkoani Mara.

Aidha katika ajali hiyo pia mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Nelson Mabeyo ambaye alikuwa rubani wa ndege namba 5H-AAM ya kampuni ya Auric air alipoteza maisha.

Akizungumza katika ibada hiyo jana iliyofanyika katika Usharika wa Sasi mtaa wa Ilmeshorori, Dayosisi ya Kaskazini Kati,Dk.Masangwa aliwapa pole wazazi na ndugu wote walioguswa na msiba huo na kuwataka kuwa na utulivu katika kipindi hicho cha majonzi.

"Binadamu siku zetu za kuishi hapa duniani fupi na zimejaa dhiki,hivyo hakuna ambaye ajuaye siku wala saa ya kifo kitakapompata, kutokana na fumbo hili inatupasa kila mmoja kukesha tukiomba,"alisema

Alisema ajali za ndege zinasababishwa na mambo mbalimbali kuanzia inaporuka,ikiwa angani na inapotua hivyo ni suala la kumwachia mungu.

"Baadhi ya sababu hizo ni makosa ya rubani,matatizo ya kiufundi,hali ya hewa,vyuma,wakati wa ndege kupaa na wakati wa kutua,huweza kusababisha ajali katika hili hakuna wa kulaumiwa,"alisema

Aidha alisema katika mazingira hayo huwezi kumlaumu mtu yoyote sababu hata rubani akijitahidi kukwepa ajali lakini bado mazingira ya ajali yanaweza kuwepo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alitoa salamu za pole kwa niaba ya serikali na kusema kazi ya mungu haina makosa.

"Huyu Nelson angemaliza safari ya masomo yake angetusaidia sana Serikali na taifa,lakini makusudi ya mungu lazima yatumike na tumwachie yeye,"alisema

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya,ametoa pole na kusema hakuna mwenye jibu kwanini mtu mwenye umri mdogo kama walivyo vijana hao waliofariki katika ajali hiyo na katika kipindi hiki ambacho wazazi wao walikuwa wakiwahitaji kuliko kipindi chochote.

"Mahali salama na pekee ni kujikabidhi mikononi mwa mungu,"alisemaKatibu wa Chama cha Marubani nchini,Khalid Lqbal amesema marehemu alikuwa mpole,mnyenyekevu, msikivu ba mwenye kupanga kujifunza zaidi.

"Hivyo tumepoteza kijana mdogo ambaye angekuja kuwa msaada hapo baadaye,"alisemaPia amesema vifo vya vijana hao Nelson Olotu na Nelson Mabeyo ni pigo kubwa kwa taifa na sekta ya masuala ya anga.


Kwa upande wa kaka wa marehemu aliyesoma histori fupi ya marehemu,Calvin Olotu alisema marehemu alisoma shule ya Msingi Trust St.Patrick mwaka 1998 na kumaliza 2009 na Sekondari ya Duluti ambayo alimaliza mwaka 2013.

Baada ya hapo alijiunga shule ya Urubani mwaka 2014 katika Chuo cha Aviation College Dar esalaam na kuhitimu mwaka 2015 kisha alikwenda kujiunga na Chuo cha urubani Nairobi nchini Kenya cha PRO-ACTIVE AVIATION COLLEGE na kuendelea na ground School na Flight mpaka mwaka 2019.

Calvin alisema marehemu alikuwa mtoto wa tatu katika familiya ya mzee Wilberd Phillemon Olotu na mauti yalipomkuta akiwa safarini katika Hifadhi ya Serengeti na amezikwa nyumbani kwa wazazi wake Kambi ya Chupa Wilaya ya Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...