BENKI
ya NMB, imewahakikishia askari wa Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa
Serikali nchini, huduma bora, rafiki na sahihi za kibenki, zitakazokuza
pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, ili kuendana na kasi ya
maendeleo kuelekea Uchumi wa Kati.
Ahadi
hiyo imetolewa na Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi na Kati wa NMB,
Ally Ngingite, katika siku ya pili ya Kikao Kazi cha Maofisa Waandamizi
wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Mikoa na Vikosi,
kinachofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es
Salaam.
Kikao
Kazi hicho kiliozinduliwa Septemba 24 na Inspekta Jenerali wa Polisi
(IGP), Simon Sirro, kimefika ukomo jana Ijumaa Septemba 27, 2019 ambapo
kwa siku nne maofisa hao wamejadili juu ya mafanikio, changamoto na
mikakati ya Kamisheni katika Kuzuia, Kupambana na Kutanzua Uhalifu.
Kupitia
Kikao Kazi hicho kinachofanyika chini ya Kaulimbiu: Umoja Wetu Ndiyo
Nguvu Yetu, Tudumishe Usalama Katika Uchumi wa Viwanda, wadau wa Jeshi
la Polisi wamealikwa kushiriki, ikiwemo NMB iliyotoa ahadi ya
ushirikiano wa kudumu, sambamba na huduma bora kwa askari polisi nchini.
Ngingite
aliwataka maofisa na makamanda hao kuwa mabalozi wema wa benki hiyo kwa
askari walio chini yao kote nchini na kwamba wanapaswa kuifanya NMB
kama mshirika wa kweli katika kujikweza kiuchumi kupitia mikopo na aina nyingine za uwezeshaji kutoka katika benki hiyo.
“Makamanda
na maofisa wote mlioshiriki Kikao Kazi hiki, mkitoka hapa huku
mnafikiria namna sahihi ya kuboresha maisha yenu ya sasa na baadaye,
kukuza pato lenu kuelekea Uchumi wa Kati, maana yake ni kuwa askari wote
nchini walioko chini yenu watafikia kufanya hivyo pia.
“Unafuu
wa huduma zetu kwa Askari wa Jeshi la Polisi, majeshi mengine na
Wafanyakazi wa Serikali, unatokana na ukweli kwamba tunatambua,
kuthamini na kujali mchango wenu kwetu kama taasisi ya kifedha,” alisema
Ngingite,
ambaye alipokea maoni mbalimbali kutoka kwa makamanda hao.
Aliwaomba
askari hao wanapoamua kukopa, kuhakikisha wanaitumia mikopo hiyo kwa
usahihi, na kwamba siri ya mafanikio iko katika kufikiria kabla ya
kukopa, kufanya uwekezaji mdogo baada ya kukopa ili kutanua pato lao na hatimaye kupunguza makali ya marejesho.
Akizindua
Kikao Kazi hicho juzi, IGP Sirro aliwataka askari hao kuhakikisha
wanajitoa kadri wawezavyo katika kulitumikia taifa na kwamba yeye
anatamani kumaliza nafasi yake Jeshi likiwa na heshima, ambayo
itapatikana kwa kila mmoja kuacha unafiki, kwani likichafuka, watachafuka wote.
Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali- Vicky Bishibo pamoja na Afisa wa benki NMB Getrude Mallya wakiwa ba baadhi ya Makamanda wa Mikoa.
Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali- Vicky Bishibo pamoja na Afisa wa benki NMB Getrude Mallya wakiwa ba baadhi ya Makamanda wa Mikoa.
Kutoka kushoto: Kamishna wa Police, Operesheni na Mafunzo- Liberatus Sabas, Kamishna Msaidizi Mwandamizi: Mipango na Bajeti- Yustus Kamugisha, Kamishna wa Polisi ; Inteligensia - Charles Mkumbo ; Kamishna Msaidizi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha - Jonathan Shana katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa Benki ya NMB-Vicky Bishubo baada ya kikao kazi cha Maofisa wa Polisi kilichofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay,Dar es Salaam.
Maafisa wa Benki ya NMB Ally Ngingite(Kushoto) na Isaac Mgwassa wakibadilishana mawazo na Kamishna Msaidizi;Tathmini na Ufuatiliaji- Semiyono
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro;S R Handuni akifurahia jambo na Afisa wa benki ya NMB Amanda Feruzi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...