Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika Masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki ameutaka uongozi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kutembelea na kukagua  mazingira ya wafanyabiashara na wawekezaji wazawa waliopo mkoa wa Ruvuma ndani ya siku saba.

Ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua kiwanda cha kutengeneza kahawa cha Wilaya ya Mbinga cha MCCCO pamoja na kiwanda cha DAE kwa lengo la kukagua mazingira na utendaji wa viwanda hivyo Mkoani Ruvuma.

Ziara hiyo iliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Christina Mdeme pamoja na watendaji kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Wizara ya Viwanda, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Nishati, Wizara ya Madini, Wizara ya Ardhi, pamoja na baadhi ya taasisi za serikali ikiwemo na Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC)

Waziri Kairuki alitoa maelekezo hayo baada ya kubaini kuwa taasisi hiyo haijawafikia wawekezaji wazawa kikamilifu hususani waliopo mikoani ili kuwatambua na kuwaeleimisha kuhusu fursa zinazotolewa na taasisi hiyo.

“Ninawaagiza TIC mfike katika viwanda hivi ndani ya siku saba kuanzia sasa ili kuwatembelea na kuwaeeleza huduma zinazotolewa na taasisi yenu ikiwemo fursa zilizopo na endapo wataona inafaa wajisajiri kwa kuwa ni suala la hiari,”alisisitiza Waziri Kairuki

Aidha alieleza kuwa ipo tija ya kuwatambua wawekezaji wazawa waliopo nchini ka kuzingatia mchango wao katika uchumi wa viwanda kwa kuzingatia mwaka huu 2019 ni mwaka wa uwekezaji.

“Naelewa kuwa ipo miradi mingi iliyofikiwa na TIC zaidi ya asilimia 72 hivyo niwatake mfike haraka mkoani Ruvuma hususan katika viwanda hivi vya kahawa, ili kuvitambua na kueleza fursa na umuhimu wa kujisajili na Taasisi hii ili kuendelea kuchangia na kuwa na tija zaidi katika uchumi wa nchi,”alisisitiza

Mkurugenzi wa sera mipango na utafiti wa TIC Mafutah Bunini amesema katika kuboresha utendaji wao wamefungua ofisi za kanda saba ili kuwafikia kwa urahisi wawekezaji wa ndani na kwamba wanaotoa uzioto sawa kwa wawekezaji wa ndani na nje.

“Na katika hili ndio maana viwango vya mitaji ya uwekezaji vinatofautiana kwa wawekezaji wa nje na ndani ambapo mwekezaji wa ndani anatakiwa awe na mtaji wa dola laki moja lakini mwekezaji wa nje ni dola laki tano
Naye meneja wa kiwanda cha kutengeneza kahawa cha wilaya ya Mbinga (MCCCO) amemuahakikishia Waziri kuwa wataendelea kuboresha mazingira mazuri ya wafanyakazi na kuongeza thamani ya bidha zao za kahawa na kuhakikisha jamii iliyowazunguka inanufaika na kiwanda hicho.

“tunaishukuru Wizara ya Uwekezaji kwa jitihada inazofanya za kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuondoa vikwazo mbalimbali vilivyokuwepo awali hali inayosababisha uwekezaji kukua kwa kasi”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kutengeneza kahawa cha DAE Bw. Danistan Komba ambaye pia ni mkulima wa kahawa alimpongeza waziri kwa kutembelea kiwandani hapo na kueleza changamoto za masoko ya kahawa na kuiomba Serikali kuendelea kuwaangalia wawekezaji hao wazawa.

“Kipekee napongeza ujio wako, japo tunachangamoto ya masoko kwa kuzingatia kiwanda kina uwezo wa kuzalisha tani 36,000 kwa mwaka na kuuza katika baadhi ya nchi ikiwemo.Alifafanua kuwa, pamoja na changamoto za uhaba wa masoko, kiwanda kimekuwa kikishiriki katika maonesho ya nchi zinazolima kahawa ikiwemo Kenya, Uganda,Rwanda,Burundi na Ethiopia.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye alieleza kuwa, ziara hiyo imeleta chachu kwa wafanyabiashara na wawekezaji wazawa kwa kuzingatia kuwa, Serikali imeahidi kutoa ushirikiano wa kina katika kutatua changamoto zao ikiwemo kuwataka TIC kufika na kuwatembela katika muda alioagiza.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akisikiliza maelezo kuhusu namna ya kuhifadhi kahawa kutoka kwa Afisa Masoko wa kiwanda cha kutengeneza kahawa cha MCCCO Bw. David Haule katika kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akikagua kahawa iliyokobolewa katika kiwanda cha kukotengeneza kahawa cha MCCCO kilichopo Wilaya ya Mbinga mkoani Songea wakati wa ziara yake kiwandani hapo.

Fundi wa mitambo ya kukobolea kahawa katika kiwanda cha MCCCO, Kelvin Moses akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki namna kahawa inavyotengenezwa katika kiwanda cha kutengeneza kahawa cha MCCCO Wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akiangalia namna kahawa iliyokobolewa inavyohifadhiwa katika magunia yanayotengenezwa na kiwanda cha MCCCO wakati wa ziara yake kiwandani hapo.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na watumishi wa kiwanda cha kutengeneza kahawa cha DAE kilichopo katika Wilaya Mbinga alipotembelea kukagua mazingira ya wawekezaji nchini.Kulia aliyekaa ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe.Cosmas Nshenyi

 Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza kahawa cha Wilaya ya Mbinga cha MCCCO wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati akizungumza nao alipotembelea kiwandani hapo.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akipokea zawadi ya kahawa kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha MCCCO Bw.Jonas Mbunda wakati wa ziara yake kiwandani hapo.


Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe.Cosmas Nshenyi akieleza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki alipotembelea kiwanda cha kutengeneza kahawa cha DAE kilichopo wilayani humo mkoa wa Ruvuma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika Masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki akiweleza jambo wawekezaji waMgodi wa Makaa ya Mawe ya kutoka kampuni ya Mil Coal,Mbinga mkoani Ruvuma. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika Masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki amkimsikiliza mmoja wa Wakulima wa zao la Kahawa,wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika Masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki akipewa maelezo kwenye moja ya kiwanda  kinachotengeneza tengeneza kahawa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma 
 Meneja wa Kiwanda cha kutengeneza Kahawa cha Wilaya ya Mbinga (MCCCO) Mhandisi Rabbian Uromi akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki kuhusu mitambo ya kutengeneza mifuko (magunia) ya kuhifadhia kahawa katika kiwanda hicho kilichopo Mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake Septemba 23, 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...