Kampuni ya Petrobena inayosambaza pembejeo za kilimo nchini, imeungana na BASF Tanzania Limited kusambaza n viatilifu na madawa vyenye ubora kwa wakulima ili kuongeza tija katika uzalishaji mazao nchini. 

Kampuni mbili hizo  zimetiliana saini mjini hapa makubaliono ya kuwa na ushirikiano huo baada ya mafunzo kwa maafisa kilimo wa kampuni ya Petrobena juu ya matumizi bora ya madawa ya kilimo yanayotengenezwa na BASF, ambayo ni kampuni ya kimataifa inayotengeneza viatilifu na aina nyingine za madawa ya kilimo. 

 Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makubaliano hayo, Afisa Mkuu Mauzo wa BASF kanda ya Afrika ya Mashariki, Bw.Lincholn Asembo, ameyaeleza makubaliano hayo kuwa ni chachu katika kuboresha uzalishaji mazao nchini Tanzania. 

 “Kampuni ya PETROBENA imekuwa ni mdau mkubwa katika kuchagiza mapinduzi ya kilimo Tanzania, hivyo ushirikiano huu utasaidia kuinua uzalishaji na kukuza kipato cha wakulima kupitia kilimo,” amesema Bw. Asembo.

 Amesema kilimo nchini Tanzania kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo wadudu waaribifu wa mazao, na kuongeza kuwa viutilifu kutoka BASF vinalenga kuondoa tatizo hilo. “Tunayofuraha kufanya kazi na Petrobena kwani ndio kampuni pekee ambayo itasambaza viuatilifu vyenye ubora wa hali ya juu nchini Tanzania. 

Lengo kubwa la kampuni yetu ni kumwinua mkulima kwa kuongeza tija kwenye kilimo kwa kutumia viuatilifu bora kutoka BASF”, amesema Bw. Asembo 
Ameeleza kuwa kampuni ya PETROBENA inamtandao mkubwa na uzoefu katika usambazaji wa mbolea hivyo haitakuwa ngumu kwao kusambaza viuatilifu ambavyo vitamsaidia mkulima kuongeza tija katika shughuli yake ya kilimo. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PETROBENA, Bw.Peter Kumalilwa, ameishukuru kampuni ya BASF kwa kukubali kufanyakazi na kampuni yao ili kwa pamoja kushiriki katika kuimarisha mapinduzi ya kilimo nchini. 
 “Tunafuraha kuanza kufanya kazi na kampuni kubwa ya kimataifa ya BASF yenye kutengeneza viuatilifu vyenye viwango vya hali ya juu ambavyo vikitumiwa vizuri vitakuwa ni mkombozi wa mkulima. 

Lengo la serikali sasa hivi ni kuinua tija katika kilimo ili wakulima wauze malighali bora kwa viwanda nchini na ziada isafirishwe nje ili kuliingizia taifa fedha ya kigeni,”amesema Bw.Kumalilwa 


Kwa kuwa Petrobena ndiyo itakuwa msambazaji mkuu wa viatilifu vya BASF nchini na ina uzoefu na weledi wa kuwahudumia wakulima, ameeleza Bw Kumalilwa, basi mkulima atakuwa na uhakika wa kupata mbolea na viuatilifu kwa wakati na pia kupata elimu ya kutumia vitu hivyo. 

 Kampuni ya PETROBENA pamoja na kusambaza pembejeo za kilimo pia hutoa mafunzo kwa wakulima kupitia mashamba darasa ili kukuza uelewa wa wakulima juu ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo ikiwemo viuatilifu na mbolea kutoka Kampuni ya Yara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...