Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),  Dk Indiael Kaaya amewataka walimu, wazazi na walezi kuwajengea watoto uwezo wa  kutambua kuwa hakuna mbadala wa kujituma na nidhamu hataka kama umezaliwa katika familia yenye kila kitu.

Dk. Kaaya ameyasema hayo wakati wa mahafali ya tano  ya shule ha msingi ya New Version ya Kibaha nje ya mji wa Dar es Salaam

“Natamani watoto wajue hakuna mbadala wa kujituma na kuwa na nidhamu  kwa sababu kila aliyefanikiwa katika maisha kuna wakati alijituma na kujinyima hivyo ukipata nafasi ya kufanya kitu iwe shule ama ofisini fanya kwa ufanisi na bidii yako yote  na nidhamu ya kujua unachotaka kukifanya ukifanye kwa wakati gani”Amesema

Amesema katika dunia hii, kunamabadiliko mengi sana yanayotokea  kwa sababu dunia imekuwa na ushindani  hasa kipindi hiki nchi inapoelekea katika mapinduzi ya nne ya viwanda ambayo teknolojia imechukua nafasi kubwa.

Wazazi, walimu wanatakiwa kuwasaidia watoto kutumia vipaji vyoa kwa sababu watu wengi waliofanikiwa na kufikia malengo yao ni wale ambao wanachanganya elimu waliyonayo na vipaji vyao. Hivyo ukiona mtoto wako anapenda kufanya kitu Fulani ikiwemo kupika mpe fursa na utengenezee mazingara ambayo yatamfanya alipate madhara.

Kwa kuwa hadi sasa kuna shughuli ambazo tayari zimeishaitishwa  kwa kufanywa na maroboti hivyo  ili mtu aweze kushindana na mabadiliko hayo yanayotokea kila siku  dunia  ni lazima awe amechanganya  elimu na kipawa chake atakuwa mtaada kwa familia taifa na dunia kwa sababu roboti halina kipawa.

Pia dk, Kaaya amewaasa wazazi nchini kujitahidi  kuwawekea watoto mipaka ya simu, na siyo watoto tu hata watu wazima kwa sababu wakimezwa na simu ni lazima wapoteze  ufanisi katika shughuli zao za kila siku na kuleta madhara na amewahamasisha kuwasaidia  watoto kuishi katika maadili ya kumjua mungu, kujitambua na kujua maono yao ili wakikua wajue wanataka kuwa akina nani.

Kwa upande wa Mkuu wa Shule hiyo, Zulfa Lema amesema shule hiyo imekuwa ikifanya mitihani ya kitaifa na kushika nafasi tatu bora wilaya na mkoa wa Pwani na mwaka 2017 ilifanikiwa kushika nafasi ya 96 kitaifa na mwaka jana ilishika nafasi ya 175 kitaifa.

Malengo tuliyojiwekea tangu shule kuanzishwa yao si kufaulisha watoto tu bali kuhakikisha vijana wetu wanapata nafasi katika shule za watoto wenye vipaji maalum jambo ambalo limekuwa likitokea mwaka hadi mwaka. Ni maombi yetu hata vijana wetu waliomaliza eli yao ya msingi mwaka huu nao wapate nafasi hizo adhimu.

Na hiivyo kuendelea kuweka juhudiu katika kuelimisha watoto ili kufikia nafasi za juu zaidi na kwamba shule hiyo tangu ianzishwe hadi mwaka uliopita haijawahi mtoto hata mmoja kufeli.

“Kutokana na mwendelezo wa matokeo mazuri mwaka 2017 waziri wa elimu Profesa Joyce Ndalichako  alitutunuku cheti ikiwa ni shule ya msingi bora kitaifa miongoni mwa shule ya mtu binafsi.

Kwa upade wa Meneja wa Shule, Magreth Moshi alisema watoto waliosoma katika shule hiyo wamefunzwa kufanya kazi hivyo watakapokuwa huko majumbani wazazi wahakikishe wanawaendeleza kuwa hivyo.
 Mmoja wa wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi wa shule ya New Version, akipeana Mkono na Mkurugenzi wa Shule ya msingi na awali ya New Version,  Andrew Madunda baada ya kupokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi. ambaye ni mhadili wa chuo cha usimamizi wa Fedha IFM Dk Indiael Kaaya hayupo pichani.
 Mhadhili wa Chuo cha usimamizi wa Fedha IFM, Dk. indiael Kaaya akizungumza wakati wa mahafali ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi na awali ya New Version iliyopo nje ya kidogo na mji wa Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...