Na Editha Karlo wa michuzi Tv,Kigoma

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya ushirika kutoingia katika uongozi huo kwa lengo la kujinufaisha kwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu haraka.

Maganga ameyasema hayo Mkoani hapo, wakati akikabidhi kadi za Mfuko wa bima ya afya(NHIF)kwa wanachama wa vyama vya ushirika kwenye mkutano mkuu wa jukwaa la maendeleo ya ushirika.

Alisema kuwa kuchezea vyama vya ushiriika kwa Tanzania ya sasa ni kama kuchezea umeme kwa kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa papo hapo.

“Kuna watu wakiona wamechaguliwa kwenye uongozi wa vyama vya ushirika wanaona kama wamepata ulaji, kumbukeni vyama hivi vilianzishwa na Baba wa Taifa letu marehemu Julius Nyerere sasa Tanzania imeamua kuvifufua, kuvichezea ni kama kuchezea umeme” Alisema Maganga.

Awali akibidhi vitambulisho kwa viongozi wa vyama vya ushirika kwa niaba ya wanachama wao alisema, enzi za nyuma matibabu yalitolewa bure lakini kwa sasa matibabu yanalipiwa hivyo kuwa na kadi ya Bima ya afya unakuwa na uhakika wa matibabu hata kama hauna pesa mfukoni taslimu pale unapougua.

"Kwakweli nawapongeza kwa uamuzi wenu wa kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwaajili ya kupata matibabu,ugonjwa unapokuja hauna taarifa unaweza kuugua huna pesa mfukoni lakini kama una kadi ya bima ya afya utakuwa na uhakika wa matibabu na dawa"alisema Maganga

Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Kigoma Benard Katerangabo alisema NHIF imelenga kutoa huduma kwa watanzania wa kawaida ambapo Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasimu Majaliwa Kasimu mwaka jana alizindua utaratibu wa wakulima wanaolima mazao ya kimkakati kama korosho,tumbaku,kahawa na mengine ambao wapo kwenye vyama vya ushirika kujiunga na mfuko wa bima ya afya kupitia ushirika afya.

Alisema wameanza na kundi la vyama vya ushirika ili kuhakikisha kuwa wananchi wanajihusisha na kilimo cha mazao ya kimkakati nchini wanafikiwa na huduma za mfuko.

Katerangabo alisema kuwa wanachama wa vyama vya ushirika watakapo jiunga na huduma za mfuko na wategemezi wao ambao ni waume, wake, watoto, wazazi pamoja na wakwe nao pia watanufaika na huduma.

Alisema kundi la wakulima ni kubwa ukiangalia Mikoa yote ya Tanzania inayolima mazao kwa kupitia utaratibu waushirika hivyo watanzania walio wengi watafikiwa na huduma za mfuko.

Akizungumzia suala la malalamiko ambayo yamekua yakijitokeza kwa wanachama wa mfuko huo kuhusu kusumbuliwa wakati wa kupatiwa matibabu alisema, mfuko huo umeweka waratibu kila Wilaya kuwa na mratibu ili kuratibu changamoto zinazojitokeza kwa wanachama wao na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati.

Alisema wakulima wa zao la tumbaku kwa Mkoa wa Kigoma wameonyesha muitikio mzuri wa kujiunga na mfuko mpaka sasa jumla ya wanachama 600 wamejiunga na mfuko huo huku wanachama 480 wakikabidhiwa kadi zao anaamini baada ya hapo idadi ya wakulima kujiunga ushirika afya itaongezeka.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akimkabidhi vitambulisho vya bima afya vya ushirika afya mmoja wa viongozi wa wanachama wa ushirika katika mkutano mkuu wa jukwaa la maendeleo ya ushirika.
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akimkabidhi vitambulisho vya bima afya vya ushirika afya mmoja wa viongozi wa wanachama wa ushirika katika mkutano mkuu wa jukwaa la maendeleo ya ushirika.
 Wajumbe wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
Wajumbe wa mkutano mkuu wa vyama vya ushirika waliohudhuria mkutano mkuu wa jukwaa la maendeleo ya ushirika kwenye ukumbi wa NSSF Kigoma mjini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...