Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dkt.Edwin Mrema akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali za majeruhi wa ajali ya moto wanaoendelea kupatiwa matibabu.
 Kutoka kulia ni Shabani Abdalla Omary na Mikidaki Issa ambao ni majeruhi wa ajali ya moto walioruhusiwa leo wakiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari na wauguzi waliowahudimia.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

MAJERUHI watatu kati ya 11 wa ajali ya moto wanaoendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wameruhusiwa kutoka hospitalini leo baada ya afya zao kuanza kuimarika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Daktari Bingwa wa Upasuaji ambaye pia ni mtaalamu wa kutibu majeraha ya moto Dkt. Edwin Mrema, amesema kuwa majeruhi hao wameruhusiwa kwa kuwa afya zao zimeanza kuimarika na kuelekeza kuwa watahitajika kuhudhuria kliniki ya wagonjwa wa nje ili kufuatilia maendeleo ya afya zao.

“Hadi kufikia leo tuna wagonjwa kumi na moja miongoni mwao ni hawa wawili na mmoja ataruhusiwa kesho, hawa wagonjwa tuliwapokea wakiwa katika hali ya hatari zaidi lakini leo tumefikia hatua ya kuwaruhusu kwenda nyumbani maana yake hali ya hatari waliyokuwa nayo imetoka, na sehemu kubwa ya vidonda walivyokuwa navyo vimepona, upumuaji wao ni nzuri na afya zao kwa ujumla zinaruhusu, lakini wataendelea kuja Hospitali kuhudhuria kliniki ya nje” alifafanua Dkt. Mrema.

Pamoja na kufuatilia mwenendo wa matibabu yao, amesema wataendelea kuhudhuria kliniki ya saikolojia ili kuwahimairisha zaidi kifikira. 

Dkt. Mrema amesema wagonjwa wameanza kupatiwa huduma za mazoezi ya viungo (physiotherapy) kwani majeraha ya moto walioyapata yanaweza kusababisha baadhi ya viungo visikae sawa.

Aidha, Dkt. Mrema amesema kuna wagonjwa wawili ambao kutokana na kuugua sana ilibidi kuwafanyia upasuaji kuondoa baadhi ya viungo ili kuokoa maisha yao,lakini kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri.

Katika hatua nyingine, mmoja wa majeruhi aliyeruhusiwa Bw. Shabani Abdalla Omary amemshukuru kwa dhati Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwatembelea hospitali hapo pamoja na kuwagharamia gharama zote za matibabu na pia ameshukuru madakrati na wauguzi wa MNH kwa huduma nzuri waliyowapa kipindi chote cha matibabu.

“Namshukuru Rais, alifika kutuona na akatupatia kiasi cha fedha Mungu ambariki sana sina cha kumlipa, lakini pia nawashukuru sana wauguzi na madaktari wa MNH kwa sababu nilivyofika hapa nilikuwa na hali ngumu mno ila kwa sasa naendelea vizuri” amesema Bw. Omary.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...