Mratibu wa Shirika lisilokua la kiserikali la INFOY ,Laurent Sabuni
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
MRATIBU wa Shirika lisilokua la kiserikali la infoy Laurent amewataka Vijana wa Kitanzania kuchangamkia fursa ya kuongeza thamani mazao na kuyafungasha katika viwango vya ubora wa hali ya juu ili yaweze kukubalika katika masoko ya ndani ya nje
Sabuni amesema hayo katika mkutano wa wadau kutoka asasi za kiraia zinazojishughulisha na vijana ambazo zinafadhiliwa na The Foundation for Civil Society ambapo amesema kuwa wamekua wakitoa mafunzo ya usindikaji wa bidhaa za chakula hususan lishe pamoja namna ya kuzifungasha bidhaa hizo ili kupanua wigo wa fursa kwa vijana.
"Vijana licha ya kujishughulisha na ujasiriamali pia wanapaswa kuongeza thamani ya mazao ya nafaka kama mahindi,ngano na hata mazao ya mifugo kuyachakata na kuyafungasha vizuri na kuyafikisha sokoni yakiwa katika hali nzuri ya kuvutia masoko ya ndani na nje" Alisema Sabuni
Kwa upande wao vijana Fransisca Wilson amesema kuwa tayari wameanza kutengeneza unga wa lishe kwa kutumia nafaka hivyo kuwasaidia kuinua kipato chao na kuchangia maendeleo katika jamii zao.
Leonard Paulo amesema kuwa mwamko wa vijana katika kuongeza thamani umeongezeka huku changamoto kubwa ikiwa ni mtaji wa kuanzia biashara zao na kununua mazao kwa kulima pamoja na mashine za kuchakata mazao na kutengeneza bidhaa.
Afisa Vijana na Maendeleo Jiji la Arusha Hanifa Ramadhani alisema kuwa vijana hao wanapaswa kusindika bidhaa za nafaka na kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo zinahitajika katika jamii badala ya kuacha mazao ya wakulima wakati mwingine yamekua yakiharibika kwa kukosa soko Na pia kutokuongezwa thamani jukumu ambalo inapaswa lifanywe na vijana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...