Ushahidi upande wa utetezi wa kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi umeendelea leo kwa utetezi wake mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Malinzi amedai kuwa fedha alizolipwa na TFF, alilipwa kihalali.
Akiongozwa na Wakili wa utetezi Richard Rweyongeza mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Maira Kasonde, Malinzi alidai kuwa dola za Marekani 2,400 alizolipwa na TFF ilikuwa ni malipo baada ya kuhudhuria mkutano wa FIFA nchini Mexico, Mei 16, 2016, ambapo wakati anaenda katika mkutano huo alitumia fedha zake mfukoni, hivyo aliporudi nchini alilipwa fedha hizo.
Amedai kuwa, malipo ya dola za kimarekani 7,000 anazodaiwa kujipatia kwa njia ya udanganyifu, alilipwa kilahalali na TFF, baada ya kuchukua fedha yake mikononi kumlipa Kocha wa timu ya vijana kiasi cha dola 7,000.
" TFF walinilipa dola za kimarekani 7,000 kwa sababu niliikopesha TFF na kumlipa mshahara kocha wa timu ya taifa ya Serengeti Boys, Kim Paulsen, kipindi hicho TFF haikuwa na fedha " alidai Malinzi.
Malinzi amedai hata dola za kimarekani 10,000 alizolipwa na TFF, alilipwa kihalali kwa sababu aliikopesha TFF ambazo alitoa mfukoni mwake kwa ajili ya kuilipia timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 walikuwa wanacheza na timu ya vijana ya Misri na hiyo ilikuwa Juni 16, 2016.
"Nilikuwa natoa fedha zangu mfukoni kuwalipa wachezaji halafu baadaye fedha zikipatikana TFF inanilipa, hivyo niseme tu fedha hizo nilipewa kihalali na TFF na wala sikujipatia kwa njia ya udanganyifu kama jinsi shtaka la 26 linavyoeleza kuwa nilijipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu" amedai Malinzi.
Mshtakiwa huyo ameendelea kujitetea kuwa katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2016, ameikopesha TFF kiasi cha Sh 320 milioni.
"Katika kipindi changu, walikuwepo watu mbalimbali ambao walikuwa wakiikopesha TFF, lakini mimi ndio Rais wa kwanza wa TFF ambaye nilikamatwa na kufikishwa Mahakamani" alidai Malinzi
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF Nsiande Mwanga, Karani Flora Rauya na Celestine Mwesigwa.
Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wako rumande kwa kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji wa fedha kuwa miongoni mwa mashtaka ambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku Flora akiwa nje kwa dhamana.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...