Na Moshy Kiyungi, Tabora.
Mwanamuziki MC Hammer alijipatia umaarufu mkubwa kwa kazi yake ya muziki wa Hip hop nchini Marekani.

Alianza kufanya muziki mwishoni mwa miaka ya 1980 hadi katikati ya 1990, wakati huo haikuwa rahisi watu kushindwa kujitokeza kwenye onesho la ngoma zake kali ambao alikuwa akiimba na kunengua jukwaani.

Baada ya kuzaliwa miaka 57 iliyopita, alipewa jila Stanley Kirk Burrell, ambaye mpaka sasa anakumbukwa kwa kusaidia kwa kiasi kikubwa kuupeleka muziki wa dunia nzima na watu wakafurahia.

Aidha anakumbukwa kutokana na aina ya muziki aliyokuwa akiifanya nchini mwake Marekani na kutamba duniani kote.

Licha ya kuwa mwanamuziki, MC Hammer ni maarufu wa Hip hop ama muziki wa kufokafoka pia amewahi kuwa mnenguaji, mtayarishaji wa muziki ma mjasiriamali katika muziki.

Ni kijana miongoni mwa vijana  wa Kimarekani mwenye asili ya Afrika ambao walitumia muda wao mwingi kufungua na kuweka milango ya muziki kulekea katika faidakubwa tofauti na ilivyokuwa awali.

MC Hammer alianza kufanya muziki mwishoni mwa miaka ya 1980 hadi katikati ya 1990, wakati huo ilikuwa ngumu watu kushondwa kujitokeza kwenye shoo yake kutokana na ngoma kali ambazo alikuwa akiimba, alijaza sana kwenye shoo zake.

Wakati huo ilikuwa kama umeenda disco kujirusha halafu DJ eti asipige wimbo wake, vijana wa mjini ‘wanamfanyizia’ DJ huyo.

Vijana wengi wa enzi hizo walikuwa wakimuiga sana kwa kuimba, wengine waliona ni fahari kumuiga kwa mavazi hata uchezaji wake.

MC Hammer alitamba wakati wake na vibao  vikali vya U Can’t Touch This na 2 Legit 2 Quit.  Vibao hivyo vilitamba na kummfanya afahamike miongoni mwa wapenda muziki duniani.

Safari ya MC Hammer katika muziki ilianzia mwanzoni mwa miaka ya 1980, pale alipoona ana rap mitaani na katika kumbi zisizo na hadhi, akaamua kukopa dola 20,000 (Shilingi Milioni 45.8 za Kitanzania)  akaanzisha lebo ya Bust it Production, ikiwa na studio yake.

Baada ya kuwa na uwezo wa kurekodi kazi zake, MC Hammer alifanikiwa kutenganeza albamu yake ya kwanza iitwayo Feel Power ya mwaka 1986.

Albamu hiyo ilirekodiwa mwaka 1986 na kuachiwa mwaka uliofuatia wa 1987 akitumia studio yake mwenyewe, Nyingine ilikuwa ikiitwa Oaktown Records chini ya mtayarishaji Felton Pilate.

Albamu hiyo iliuza zaidi ya nakala 60,000 ka ilisambazwa na City Hall Records. MC Hammer pia aliachia singo yake iitwayo “Ring Em”, ambayo iklifanya vizuri wakati huo na kuzidi kumpa jina.

Kuanzi hapo studio kibao zikawa zinataka kufanya kazi na MC Hammer lakini yeye aliamua kuingia mkataba na studio ya Capital Records wa kurekodi albamu yake nyingine huku akikunja dola Milioni 1.7 ambazo sawa na Shilingi bilioni 3.9.

Fedha hizo alizopata MC Hammer aliamua kuwekeza katika mambo mbalimbali ikiwemo kampuni ya mavazi mbalimbali na biashara nyingine ili aweze kujiongezea kipato mbali na muziki.

Akiwa na Capitalm Records, mwaka 1989, MC Hammer aliachia albamu ya Let’s Get It Started, iliyouza nakala million mbili huku ikiwa na vibao vikali kama Pump It Up, Turn This Murtha Out, Let’s Get Started na They Put Me in The Mix.

Baadhi ya albamu zingine za MC Hammer ni Please Hammer, Don’t Hurt ‘Em ya mwaka 1990, Too Legit to Quit ya mwaka 1991,  New Venture ya mwaka 1992, The Funky Heahunter ya mwaka 1994, Inside Out ya mwaka 1995 na Too Tight ya mwaka 1996.

MC Hummer aliendelea kutoa albamu mbalimbali lakini singo yake ya mwisho aliitoa mwaka 2014, ikiitwa All in My Mind, aliyoimba na kundim lake la zamani la Oakland, wakimshirikisha Mistah F.A.B

Miaka hiyo ya 1990, MC Hammer aliigeukia dini na kuwa muhubiri wa dini ya Kikristo na kuendesha kipindi chake cha M.C. Hammer and Friends.

Aidha kuna mradi wake wa Katuni za televisheni ziitwazo Hmmerman, zilitoka mwaka 1991 na amewahi kuwa na kipindi chake cha kuzungumzia maisha kilichoitwa Hammertime mwaka 2009.

MC Hammer bado anapanda kimuziki, lakini wajuvi wa mambo wamesema hawezi kurejea enzi zake za zamani.


Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa mitandao.
Mwandaaji anapatikana kwa namaba: 0784331200 na 0767331200.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...