Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

MCHUNGAJI wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza (33) , na wake zake wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kuishi nchini Vila ya kibali na kufĂ nya kazi za kanisa bila kibali.

Mbali na mchungaji huyo, washitakiwa wengine ambao ni wake zake ni, Easther Sebuyange (27), Kendewa Ruth (26) na Samwel Samy (22) mdogo wake.

Mchungaji Huyo ambae hivi karibuni video yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha kuwa na wake zake watatu ambao alidai walikuwa mbioni kumtafutia mke wa nne

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa serikali kutoka idara ya uhamiaji Godfrey Ngwilo akisaidiana na Sita Shija amedai mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu Mwandamizi Agustino Mbando kuwa, Septemba 2 mwaka huu eneo la Salasala Kilimahewa, jijini Dar es Salam, mchungaji huyo na wenzake hao walibainika kuishi nchini bila kibali.

Katika shitaka la pili, linalomkabili mchungaji huyo pekee ilidaiwa kuwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa alikutwa akijihusisha na kazi za kanisa kama mchungaji akiwa hana kibali cha kuishi nchini.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, mchungaji David amekana shitaka la kwanza na kukiri shitaka la pili huku washitakiwa wenzake wakikiri mashtaka yote.

Hata hivyo, washitakiwa wote walirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama iliwataka washtakiwa hao kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 9 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...