Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira kuutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Kemilembe Mutasa akiongea na Mafundi wanaohudumia gesi za majokofu na viyoyozi wakati wa warsha ya mafunzo kuadhimisha siku ya tabaka la ozoni Duniani iliyofanyika katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Chang;ombe jijini Dar E s Salaam.
Mgeni Rasmi katika Warsha ya siku moja ya maaadhimisho ya siku ya ozone Duniani Bibi Vaileth Fumbo akiongea na Washiriki wa warsha hiyo ambayo ilifanyika katika Chuo cha VETA jijini Dar Es Salaam. Washiriki wa warsha hiyo ni Mafundi wa gesi za majokofu na viyoyozi

Sehemu ya Washiriki wa warsha ya mafunzo ya maadhimisho ya siku ya ozoni Duniani wakimskiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) warsha hiyo ilifanyika katika Chuo cha mafunzo ya Ufundi –VETA Chang’ombe

Washiriki wa warsha hiyo wakipatiwa mafunzo juu ya utunzaji wa gesi iliyotolewa kwenye jokofu na baadaye kuweza kutumiwa tena (badala ya kuacha isambae hewani na kuharibu tabaka la hewa). Gesi hiyo inatunzwa na kifaa kiitwacho recovering unit.



……………………

Utafiti wa kisayansi katika tabaka la ozoni katika karne ya ishirini ulithibitisha kumong’onyoka kwa tabaka hilo kutokana na kulundikana angani kwa kemikali aina ya chloroflourocarbons (CFCs), halons, methyl choroform, methyl bromide, carbon tertrachoridena nyinginezo. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Chuo cha VETA– Chang’ombe Bi Vaileth Mfumbwa wakati wa warsha ya mafunzo kwa Mafundi mchundo wanaoshughulikia majokofu na viyoyozi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya tabaka la ozoni Duniani iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, iliyofanyika katika Chuo cha VETA-Chang’ombe jijini Dar Es Salaam.

Aliongeza kuwa Kemikali hizi hutumika katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya kuzimia moto, ushafishaji chuma, utengenezaji wa magodoro, madawa na manukato ya kupulizia, ufukizaji wa udongo katika vitalu vya tumbaku na mashamba ya maua na ufukizaji wa mazao katika maghala kabla ya kusafirishwa nje ya nchi. Matumizi ya kemikali hizi yapo kwa wingi katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea, kama Tanzania.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bi Kemilembe Mutasa alisema kuwa , Kitaifa maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni yanafanyika jijini Dar es Salaam ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira kwa kushirikiana na Wakufunzi wa Chuo cha Ufundi Dar es salaam wamepanga kutoa mafunzo kwa vitendo kwa mafundi mchundo wanaohudumia majokofu na viyoyozi kuhusu njia bora za kuhudumia vifaa hivyo; kutoa elimu jinsi ya kutumia vitambuzi vya gesi; na kubadilisha tekinolojia zinazotumia kemikali haribifu kwa tabaka la Ozoni kwa kemikali mbadala.

“Katika maadhimisho haya, tunakumbushwa kuwa katika Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Monteral uliofanyika nchini Rwanda mwaka 2016, nchi wanachama zilikubaliana kupunguza uzalishaji na utumiaji wa kemikali jamii ya Hydrofluorocarbons (HFCs) ambazo pia hujulikana kama R-143a kwa jina la biashara na kukubaliana kuzuia ongezeko la joto la dunia kwa nyuzi joto 0.5 (0.5 degrees Celsius)” alisema Bi. Mutasa



Warsha hiyo ya mafunzo ya siku moja imekua chachu kwa Mafundi Mchundo wanaoshughulikia majokofu na viyoyozi kwa kufundishwa njia mbalimbali za kiutaalamu za kutumia wanapokua katika shughuli zao za kila siku. Mafunzo hayo yalitolewa na Wakufunzi wa Chuo cha Ufundi-VETA Chang’ombe jijini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...