Na Jusline Marco-Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Mfaume Taka amewataka wananchi kuchangamkia fursa za kukuza uchumi kwa kubadili utamaduni wa asili kuwa utalii wa utamaduni ili kuzidi kuwavutia wageni wengi.

Mhe.Taka amayesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la utalii wa utamaduni lijulikanalo kama tamasha la utalii wa utamaduni wa Masai Ngorongoro linalotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Amesema wilaya ya Ngorongoro iliweka mpango huo kwa muda mrefu baada ya kuona kuna haja ya wananchi wilayani humo kunufaika na mila na desturi zao ambazo zimetunzwa kwa muda mrefu kwa kuzibadili ili kuwezakuingiza kipato kwa wananchi.

Amesema, wilaya hiyo tayari imeshirikiana na kila mdau ambae atakuwa tayari kutangaza utamaduni wa makabila yaliyopo ili kuuenzi na kuwa kivutio bora zaidi kwa wageni hasa watalii kutoka nchi za nje wanaopenda kuona na kujifunza vitu vya asili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Trace Hills Mgema Mhina,amesema kampuni hiyo kwa kushirikiana na wilaya ya Ngorongoro imeandaa tamasha hilo ambalo litajumuisha maonesho ya mila na desturi za makabila yaliyomo katika wilaya hiyo wakiwemo Wamaasai, Wasonjo,Watindiga na Wamang’ati.

Vilevile amesema katika tamasha hilo kutakuwa na maonesho ya mavazi ya asili,mitindo ya nywele, mapambo ya asili, michoro ya asili, vyakula ,ngoma za asili za makabila hayo,kampuni za utalii, bidhaa za utamaduni ili watu mbalimbali wakiwemo wageni waweze kujifunza zaidi.

Aidha ameongeza kuwa malengo ya tamasha hilo ni kukuza utalii na utamaduni wa makabila hayo na kutambulisha kitaifa na kimataifa, kukuza uchumi kwa wananchi wa Ngorongoro na nchi kwa ujumla jambo ambalo litaweza kutuza mazingira ya hifadhi .

Naye Mzee wa Kabila la Kimaasai Wiliam Ole Seki amesema Wilaya ya Ngorongoro ndio mahali pekee ambapo mila na desturi za makabila bado zinaenziwa kwa kiasi kikubwa bila kuingiliwa na tamaduni za makabila mengine au nchi nyingine.Tamasha hilo la utalii wa utamaduni Wilayani Ngorongoro linatarajiwa kufanyika Septemba 18 hadi 20 katika kiwanja cha Waziri Mkuu Wasso Loliondo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo watalii.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Mfaume Taka akiwa na viongozi wengine akiwemo kiongozi wa kimila Mzee wa Kabila la Kimaasai Wiliam Ole Seki Wilayani humo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...