Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa akimkaribisha Mgeni Rasmi (aliyekaa) wakati wa warsha ya mafunzo kwa Maafisa Forodha na Wasimamaizi wa Sheria Nchini kuhusu udhibiti wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni. Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa CEEMI jijini Dar Es Salaam.
Mgeni Rasmi katika warsha ya mafunzo kwa Maafisa Forodha na Wasimamaizi wa Sheria Nchini kuhusu udhibiti wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Faraja Ngerageza akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa warsha hiyo.
Sehemu ya Washiriki kutoka Taasisi za Serikali wakifuatilia kwa makini wakati wa warsha ya mafunzo kwa Maafisa Forodha na Wasimamaizi wa Sheria Nchini kuhusu udhibiti wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Mgeni Rasmi katika warsha ya mafunzo kwa Maafisa Forodha na Wasimamaizi wa Sheria Nchini kuhusu udhibiti wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Faraja Ngerageza akiongea na Wajumbe waliohudhuria warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar Es Salaam.

*************************

Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Faraja Ngerageza amesema kuwa Matokeo ya kuharibika kwa Tabaka la Ozoni ni kuruhusu mionzi zaidi ya urujuani (UV-B) kufikia uso wa ardhi hivyo kutishia afya ya viumbe hai katika ikolojia mbalimbali.

Ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam wakati akifungua warsha ya
mafunzo kwa Maafisa forodha na Wasimamizi wa sheria Nchini kuhusu udhibiti wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni.

Aliongeza kuwa, Wanasayansi duniani wamethibitisha kuongezeka kwa magonjwa ya kansa ya ngozi, uharibifu wa macho kama vile "mtoto wa jicho" unaosababisha upofu, upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi na kujikunja kwa ngozi hivyo mtu aweza kuonekana mzee kuliko umri wake. Pia watoto wako katika hatari zaidi ya kupata madhara haya.

Madhara mengine ni pamoja na kuharibu fiziolojia ya mimea na
michakato ya ukuaji wake na kusababisha mabadiliko katika muundo wa spishi, hivyo kusababisha mabadiliko ya bioanuwai katika ikolojia mbalimbali

Aidha katika kuhakikisha kuwa jukumu hili chini ya Sheria ya Mazingira linatekelezwa na kusimamiwa ipasavyo Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Maafisa forodha imekuwa ikijitahidi kujenga uwezo wa Taasisi mbalimbali katika kusimamia Kanuni za Udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la Ozoni za mwaka 2007 pamoja na kutoa vifaa katika mipaka yetu vinayowezesha kutambua gesi hizi zinapoingizwa nchini.

Ofisi ya Makamu wa Rais imekua na utaratibu wamara kwa mara kuandaa warsha ya mafuzo kwa Maafisa Forodha na Wasimamizi wa sheria Nchini kote kuhusu udhibiti wa kemikali ambazo zinzingizwa Nchini zinazoharibu tabaka la ozoni.

Warsha hiyo imehudhuriwa na Maafisa forodha wa mipaka yote Nchini kutoka katika Taasisi mbalimbali za Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...