Na Karama Kenyunko, Michuzi Blog
SERIKALI imefurahiswa na hatua ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuanza kutekeleza mkataba wa MINAMATA wa kusitisha matumizi ya zebaki katika vifaa vya hali ya hewa na kuanza kutumia mitambo ya kisasa ya kidigitali kupimia hali ya hewa katika maeneo mbalimbali njia itakayopungaza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ametoa pongezi kwa TMA kwa hatua hiyo wakati  alipotembelea banda la TMA baada ya kufunga mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa, uliokuwa ukifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema serikali inaangalia namna sahihi ya kuwekeza ili kuteketeza vifaa hivyo vya zebaki kiusalama zaidi ambalo likifanikisha litasaidia sana katika kutunza mazingira ukizingatia vifaa hivyo vya zebaki ni moja kati ya vitu vinavyochangia kwa kiasi uharibifu wa mazingira.

"Vifaa vya zebaki ni hatari katika mazingira, tuko mbioni kuona ni namna gani sahihi ya kuweze kuteketeza vifaa hivyo kiusalama zaidi," amesema Mhandisi Kamwelwe

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa amesema kuwa, TMA  kwa uwezeshwaji uliofanywa na serikali Wa kupata vifaa ambavyo havitumii zebaki,  wameshafanikisha zoezi la kuacha matumizi ya vifaa vyenye zebaki vikiwemo vipima joto (thermometers) na vipima mgandamizo wa hewana tayari kuna baadhi ya maeneo vifaa hivyo vimeweza kufungwa.
 Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa akitoa maelezo kwa viongozi katika banda la TMA wakati mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akitoa ufafanuzi kwa Mh.Balozi Seif, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika banda la TMA wakati wa mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, Habari, uchukuzi na hali ya hewa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.
 Mkuu wa Taasisi ya Hali ya Hewa ya Zimbabwe Rebecca Manzou akipata maelezo katika banda la TMA wakati mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Washiriki kutoka TMA katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho katika banda la TMA wakati mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...