Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema mabweni mawili ya wanafunzi maarufu “hall 5 na hall 2 “katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam yaliyokarabatiwa  yatachukua wanafunzi  788 . Ndalichako amesema hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya ukarabati wa Mabweni, Vyumba vya mihadhara na Ofisi katika Ndaki ya Uhandisi Katika Chuo hicho.

Mabweni hayo, yanakarabatiwa na Serikali kwa Shilingi za Tanzania zaidi ya Bilioni 4.5, ukarabati ukihusisha  kuweka upya mifumo ya maji safi na taka, mifumo ya umeme, kuwekwa upya makabati na milango mipya, madirisha  uwekaji vigae vipya vya ukutani na uwekaji “lift” mpya.

Ukarabati huu unatarajiwa kukamilika, ifikapo mwezi Oktoba, 2019.  unatekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT- na kusimamiwa na  kurugenzi ya milki ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ulianza 2018. Mabweni haya yalijengwa mwaka 1965 na kwa mara ya kwanza yanafanyiwa ukarabati mkubwa baada ya kusitisha utumiaji kutokana na uchakavu.

Waziri Ndalichako amepongeza kasi na ubora wa kazi ya ukarabati huo, huku akipongeza hatua ya chuo Kikuu kutumia wataalamu wake wa ndani kusimamia kazi za ukarabati katika chuo hicho.

“Nimefurahishwa na kazi hii ni bora na  kasi ya kazi ya ukarabatiwa mabweni haya kwani  yataongeza uwezo wa chuo kutoa huduma ya Malazi kwa wanachuo zaidi ya 11,100. Naagiza uongozi mko hapa  maagizo kwa hakikisheni ukarabati wa mabweni haya na majengo katika Ndaki ya Uhandisi unakamilika kabla ya kufunguliwa Chuo Novemba  ili isiwe bugudha kwa wanafunzi, Mwaka huu ”

Akimkaribisha Waziri wa Elimu, Makamu Mkuu wa  Chuo Cha Dar es salaam Profesa  Wiliam Anangisye ameishukuru Serikali ya awamu ya tano na Waziri wa Elimu kwa kutekeleza kwa vitendo azma ya kuboresha ili ili kuhahakikisha vijana wanapata elimu katika mazingira bora. Amemuhakikishia  Waziri Ndalichako kuwa Chuo kitasimamia na kuhakikisha kazi zinazoendelea zinakamilika kwa wakati .

“ tunaishuruku serikali ya Awamu ya Tano na wewe Mheshimiwa kwani maendeleo haya ni maono ya Serikali na yanatekelezwa na serikali , nasi tunakuhakikishia pia kuendelea kutunza miundo mbinu hii na kutumia mapato ya ndani kuyaendeleza”

Nae Dkt. Liberato Haule Mkurugenzi wa Mipango Uwekezaji na Maendeleo akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi amezungumzia ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi kuwa umefikia asilimia 45 na kuwa utagharimu shilingi bilioni  1.5  .

“ napenda kutoa taarifa kuwa mradi wa ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi unahusisha  majengo ya ofisi na madarasa, nyumba za wafanyakazi na bweni moja lililopo kitalu G.  nikuhahakikishie Mh Waziri kuwa mataraji yetu ni kuwa kazi itakamilika kwa wakati uliopangwa Novemba  mwaka huu“

Nae Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) Bi. Jackline Ndombele, ameishukuru serikali kwa ukarabati mkubwa unaoendelea  hall 5 na hall 2 na kwamba utasaidia sana kuongeza idadi ya  wanafunzi wanaokaa chuo, kwani kwa sasa wengi wanakaa nje ya Chuo.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET), Prof. Aloyce Mayo, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya ukarabati wa mabweni mawili ya wanafunzi pamoja na mfumo wa kusambaza majisafi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
 Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikagua mabweni yanayokarabatiwa  katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Waziri wa Elimu,Sayansi  na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako katika ukaguzi wa mabweni katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Picha mbalimbali za ukaguzi wa majengo yanayokarabatiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...