Mtawa wa Mtawa wa Shirika la Yesu Brother Vincent Soleng (wa pili kushoto) akionesha Tuzo ya kutambua mchango wake katika utunzaji mazingira kwa kupanda miti takriban 160,000 aliyopewa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ambapo mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene. Kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Peter Claver, Padri Karongo Buberwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akipanda mti ikiwani sehemu ya kumuunga mkono Mtawa Vincent Soleng aliyepanda miti laki sita katika eneo hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akizungumza katika hafla ya kumpongeza Mtawa wa Shirika la Yesu Brother Vincent Soleng mwenye umri wa miaka 83 ambaye amepewa Tuzo na Kiongozi wa Kanisa Katiliki Duniani Papa Francis kutokana na mchango wake katika utunzaji wa mazingira baada ya kupanda miti takriban 160,000 eneo la Ihumwa ilipo Shule ya Sekondari Mtakatifu PeterClaver Jijini Dodoma.

Mtawa wa Mtawa wa Shirika la Yesu Brother Vincent Soleng akitoa neno la shukrani katika hafla ya kumpongeza kwa kupewa Tuzo ya Utunzaji mazingira na Papa Farncis.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiandaa sehemu ya kupanda mti ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Mtawa Vincent Soleng katika juhudi zake za utunzaji mazingira.


Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Peter Claver, Padri Karongo Buberwa akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene kuzungumza.


Sehemu ya wanafunzi wa wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Peter Claver wakifuatilia matukio katika halfa ya kumpongeza Brother Vincent Soleng.


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Peter Claver wakitoa buridani katika hafla hiyo.


Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Peter Claver, Padri Karongo Buberwa akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene alipowasili shuleni hapo.


Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma pamoja na wafanyakazi wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Peter Claver.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...