ALIYEKUWA Mhasibu wa Shirikisho la Soka  Tanzania (TFF), Nsiande Mwanga (29) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa hakuwahi kumsaidia Jamal Malinzi kupata fedha yoyote kwa sababu fedha zilizokuwa zikitolewa ni kwa ajili ya shughuli mbalimbali za shirikisho hilo.

Mwanga amedai hayo leo Septemba 26, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akitoa ushahidi wake wa kujitetea mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Akiongozwa na Wakili Richard Rweyongeza, Mwanga amedai alianza kazi TFF Aprili Mosi 2016 na kabla ya kujiunga na shirika hilo hakuwa anawafahamu Malinzi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa.

Alidai alipojiunga na shirikisho hilo hakuwa anafahamu kwamba walikuwa wanamtafuta mtu anayehusika na kodi na kwamba katika barua yake ya ajira ilimuelekeza poa kufanya kazi atakazopewa na mwajiri wake.

Amesema, hajawahi kuhusika na malipo ya Malinzi katika benki nyingine yoyote kwa sababu alikuwa mtia saini wa benki za Stanbic pekee na katika hundi zilizoletwa mahakamani ameweka saini hundi mbili na nyingine sijui nani aliyesaini," amedai Mwanga.

Pia amedai kuwa, anatambua Malinzi anaidai TFF kwa sababu wafanyakazi waliopo kwenye kitengo cha uhasibu wanajua kwamba Malinzi anadai ingawa yeye hajawahi kupata maelekezo yoyote kutoka kwa Malinzi akimuomba ampatie fedha na kwamba hakuwahi kuandika hundi ya kumlipa.

Pia amedai, Hellen Adam ambaye ni mhasibu wa TFF ndio alikuwa mtu wa kwanza kumpeleka benki ya Stanbic na kumtambulisha kama mtia saini na sio washitakiwa Mwesigwa na Malinzi.

Mwanga ameiomba mahakama imuachie huru kwa sababu hakuwahi kushirikiana na Mwesigwa kumsaidia Malinzi kujipatia fedha yoyote kama mashitaka ya utakatishaji fedha yanavyoeleza.

Mbali na Malinzi na Mwesigwa  washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani Flora Rauya.

Katika kesi  hiyo ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...