Wachezaji wa Timu ya Simba wakipanda gari kuelekea Hotelimara baada ya kuwasili Bukoba.
Kocha wa Timu ya Simba Patrick Aussem.
Anaadika Abdullatif Yunus - Michuzi TV.
WEKUNDU wa msimbazi Timu ya Simba Sports Club wamewasili salama Mjini Bukoba Majira ya Saa tatu kwa usafiri wa anga, tayari kuziwinda pointi tatu muhimu dhidi ya wenyeji wao Kagera sugar.
Katika hali ya isiyo ya kawaida Timu hii ya Simba imewasili kimya kimya Mjini Bukoba tofauti na miaka iliyopita, ambapo hali ya mapokezi imeonekana kuwa hafifu bila kushuhudia zile mbwembwe, shamra shamra za mashabiki licha ya baadhi ya mashabiki ndaki ndaki wa boda boda kujitokeza kuipokea Timu na kisha kuisindikiza hadi Hotelini.
Akizungumza Mara baada ya kutua katika kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Kocha wa Timu ya Simba Patrick Aussems amesema "..Timu imekuwa kambini takribani siku tatu, na tayari imewasili salama Bukoba, tutakuwa na mazoezi mepesi mchana tayari kwa mchezo wa kesho, ingawa Kagera Sugar imekuwa ikimpiga Simba, lakini Mara hii tumejiandaa.." Amesema Aussems
Picha ya Coach Aussem???????
ReplyDelete