Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. GeorgeSimbachawene akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani.
Sehemu ya washiriki wa Maadhimosho ya Siku ya Amani Duniani wakifuatiliamatukio.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiwa na viongozi wengine kuanzia kushoto ni Mkurugenzi wa Jukwaa la Mabadiliko ya Tabianchi Rebeca Muna, Mkurugenzi wa MashtakaBiswalo Mganga, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN)-Tanzania AmonManyama na Clara Makanya kutoka Shirika la Mazingira.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani Waziri wa Nchi Ofisiya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachaweneakivishwa skafu na skauti alipowasili katika tukio hilo.
Picha ya pamoja ikiwahusisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (walioka katikati)mara baada ya kuhutubia Maadhimisho hayo.

**********************


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. GeorgeSimbachawene amesema mabadiliko ya tabianchi nchi huathiri moja kwa mojashughuli za kiuchumi na ustawi wa jamii hivyo huatarisha amani.

Akizungumza kwenye kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani
yaliyofanyika Jijini Dodoma Septemba 21 Mhe. Simbachawene ambaye alikuwamgeni rasmi alisema kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi huchangiwa nashughuli za kibinadamu.

Alisema kuwa shughuli hizo husababisha kuongezeka kwa halijoto, kupunguakwa kiwango cha mvua, kukauka kwa vyanzo vya maji na kuongezeka kwamagonjwa ya binadamu, wanyama na mimea.

"Kwa kiasi kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi huchangiwa na shughuli zakibinadamu zikiwemo uchafuzi wa hali ya hewa, uchomaji misitu, ukataji miti bilakuotesha na shughuli za kilimo na ufugaji zisizozingatia uhifadhi wa mazingiraambazo huchangia kuongezeka kwa hali ya joto," alisema Waziri huyo.

Aliongeza kuwa pamoja na athari za mabadiliko haya kuzikumba nchi zote
duniani pia huzikumbwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na hi ni kutokanana ukeli kuwa ukuaji wa uchumi wetu hutegemea zaidi shughuli za kiuchumi.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo alibainisha kuwa ili kukabiliana changamotohizo kama nchi tunahitaji kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kuhimili nakujiepusha na majanga yanayosababishwa nayo.

Alitahdharisha kuwa majanga yanayotokana na hali hiyo husababisha hasara zakiuchumi na kijamii zinazochangia kuongezeka kwa umaskini na hata migogoroya kijamii.

“Chanzo cha kupotea kwa amani kwa baadhi ya maeneo ni chanzo chake ni
mabadiliko ya tabianchi na hali ikibadili watu wakakosa mahitaji kama maji
hawawezi kukubali kufa lazima watatumia nguvu yoyote kuyapata kwa
kugombana.

“Hali ya hewa ikibadilika kusababisha kukosekana kwa maji watu watapambanana kutafuta yake kidogo yaliyopo na katika kuyatafuta lazima watagombana hivyo kusababisha vurugu hivyo amani ina uhusiano mkubwa na mabadiliko yatabianchi”alisema.

Mhe. Simbachawene alidokeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa mazingirahivyo imeendelea kufanya jitihada kubwa za kutunza na kusimamia mazingirakwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ukuta wa kingo za bahari.

Kwa upande mwingine Waziri Simbachawene alihimiza jumuiya za kimataifakuweka mkazo katika kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabia nchi kwakuzingatia kuwa uchumi wetu hutegemea shughuli zitokanazo na mazingira.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN)-Tanzania Amon
Manyama alipongeza Serikali kwa jiihada zake za kulinda amani hususana katikakukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema kuwa ni jambo jema kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na
changamoto hiyo na kuwa amani ni msingi wa kuanzishwa kwa UN hivyo
tuhakikishe jitihada hizi zinadumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...