Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) linatarajiwa kutoa Tuzo za Mchezaji Bora, Golikipa Bora na Kocha Bora wa msimu wa 2018 - 2019, Septemba 23 mwaka huu.

TUZO ZA MCHEZAJI BORA WA MSIMU,
Wanaowania ni Virjil Van Dijk, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

VIRJIL VAN DIJK anawania Tuzo hiyo kwa mafanikio aliyoyapata msimu uliopita akiisaidia Liverpool kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) msimu uliopita, na alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya (UEFA).

LIONEL MESSI na yeye anawania Tuzo hiyo kwa kuisaidia Barcelona kutwaa taji la Ligi Kuu Soka nchini Hispania (La Liga) pamoja na Kiatu cha dhahabu katika Ligi hiyo.

CRISTIANO RONALDO Nyota huyo alishinda taji la La Liga na Italian Super Cup kwa mara ya kwanza akiwa na Juventus ya Italia, pamoja na hayo alishinda UEFA Nation League na Ureno.
 KOCHA BORA WA FIFA MSIMU WA 2018-2019

Wanaowania Tuzo ya Kocha Bora wa FIFA ni Jurgen Klopp, Pep Guardiola & Mauricio Pochettino.

MAURICIO POCHETTINO aliiongoza Tottenham Hotspurs katika Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) msimu uliopita licha yakufungwa na Liverpool bao 2-0 katika mchezo wa Fainali ya Michuano hiyo.

PEP GUARDIOLA yeye ameiongoza Manchester City kutwaa taji la Ligi Kuu Soka nchini Uingereza (Premier League) msimu uliopita pamoja na kutwaa taji la FA Cup, na Kombe la Ligi pamoja na Ngao ya Hisani.

JURGEN KLOPP Kocha wa Liverpool  ameisaidia timu hiyo kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) msimu uliopita na kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu Soka nchini Uingereza (English Premier League) akiachwa Points moja na Man City ambao walikuwa Mabingwa.
TUZO YA GOLIKIPA BORA WA MSIMU

Wanaowania Tuzo hiyo ni Kipa Alisson Becker, Marc-Andŕe Ter Stegen na Ederson Santana de Moraes

ALISSON BECKER ameitumikia  Liverpool na Brazil kwa mafanikio, ikiwa kutwaa Tuzo ya Kipa Bora wa Copa America msimu uliopita ambapo Brazil walitwaa taji hilo.

EDERSON SANTANA DE MORAES yeye ameisaidia Manchester City kutwaa kwa mara nyingine taji la Ligi Kuu Uingereza (EPL) msimu wa 2018-2019.

MARC-ANDRE TER STEGEN
akiwa na Barcelona ameisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu nchini humo (La Liga) na kufika hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CHAMPIONS LEAGUE).
TUZO YA GOLI BORA LA FIFA MSIMU HUU

Wanaowania Tuzo hiyo, Lionel Messi, Juan Fernando Quintero na Daniel Zsori

LIONEL MESSI anawania tuzo hiyo katika bao lake la Ligi dhidi ya Real Betis, 17 March 2019.

JUAN FERNANDO QUINTERO, Nyota wa Kimataifa wa Colombia anayecheza River Plate,  yeye anawania Tuzo hiyo kwa bao lake alilofunga dhidi ya  Racing Club mnamo 10 February 2019.

DANIEL ZSÒRI Mshambuliaji wa Debrecen FC na Romania anawania Tuzo hiyo katika bao lake dhidi ya Ferencváros TC mnamo 16 February 2019).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...