Rais wa Rwanda Mh,Paul Kagame akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni Pr.Teddy Wilson kwa pamoja wakisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye jiwe la msingi,mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa chuo hicho leo mjini Kigali,nchini Rwanda.
Picha ya pamoja mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la uzinduzi
Mandhari ya chuo kikuu cha afya nchini Rwanda kinavyoonekana mara baada ya kuzinduliwa rasmi leo mjini Kigali,nchini humo.


Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni Pr.Teddy Wilson amezindua chuo kikuu cha Afya nchini Rwanda kwa lengo la kutoa fursa ya elimu ya afya kwa wanafunzi wa Mashariki ya kati  ya Afrika. 

Hafla fupi ya uzinduzi wa chuo hicho cha afya kinachomilikiwa na kanisa la Waadventista wasabato mashariki kati mwa Afrika, limefanyika leo mjini Kigali ambapo Teddy Wilson amesema elimu bora siyo jengo bali ni huduma bora inayotolewa ndani ya majengo hayo huku akisema chuo hicho licha ya kutoa elimu ya afya inatoa huduma ya kiroho. 

Nae Rais wa Rwanda Mh.Paul Kagame amesema kwa kutambua huduma mbalimbali zinazotolewa na kanisa hilo, Serikali yake itaongeza ardhi kwa chuo hicho pamoja na fedha, huku akipongeza Makanisa ya Waadventista wasabato nchini humo kwa kuadhimisha miaka 100 ya utoaji huduma ya kijamii na kiroho nchini Rwanda,kwani huduma walizozitoa zimekuwa na matokeo makubwa katika kuleta maendeleo hasa katika sekta ya afya na elimu. 

Awali akiwasilisha taarifa fupi ya chuo hicho Mwenyekiti wa jimbo la Afrika Mashariki na kati mchungaji,Dkt  Blasous Luguri alieleza kuwa mpaka  kukamilika kwa ujenzi wa chuo hicho, kitasaidia kutoa mchango mkubwa wa elimu ya afya nchini humo. 

Uzinduzi wa chuo hicho umeshuhudiwa na viongozi wa Serikali ya Rwanda akiwemo Waziri wa Afya nchini humo Diana Lumba, Waziri wa Elimu Eugene Tamura pamoja na viongozi mbalimbali wa kanisa la Waadventista wasabato divisheni ya Afrika. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...