Na Woinde Shizza - Globu ya Jamii, Arusha
Katibu tawala mkoa wa Arusha, Richard Kwitega amewataka wakulima kote nchini kuyaenzi matumizi ya mbegu za asili ili kuepuka tishio la kutoweka kwa mbegu hizo kutokana na mwingiliano wa matumizi ya mbegu mpya zinazoonekana kushamiri kwa wingi kwa wakulima.
Rai hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki katika maonyesho ya mbegu na vyakula vya asili yaliyoandaliwa na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima MVIWATA na kufanyika kwa siku moja wilayani Karatu, ambapo wakulima kutoka mikoa mbalimbali nchini walifanya maandamano na kuonyesha mbegu za mazao mbalimbali ya asili.
Aidha alisema changamoto nyingine inayoikumba mfumo huo wa mbegu usio rasmi ni pamoja na kutofika kwa wakulima kwa wakati kutokana na uratibu na usambazaji usio wa uhakika hivyo kupelelekea wakulima kutumia mbegu za kisasa katika kilimo .
Alibainisha kupuungua kwa uhifadhi wa mbegu unaosababishwa na ukame hivyo ambapo amewataka wakulima kutumia maonyesho hayo kupanua wigo kwa wakulima ila kutatua changamoto hizo za utumiaji na upatikanaji wa mbegu za asili.
mratibu wa MVIWATA Mkoa wa Arusha, Richard Masandika amesema kuwa kupitia mradi wao wa kilimo endelevu sheria ya mbegu ya mwaka 2016 imekuwa kikwazo kikubwa kwa wakulima katika kutekeleza mfumo wa mbegu za asili na kuitaka serikali itazame upya sheria hiyo ili matumizi ya mfumo usio rasimi yaweze kutambulika na kufufua matumaini mapya kwa mkulima.
Amesema kuwa wadau wa kilimo endelevu waliamua kuwasaidia wakulima kupunguza kero ya upatikanaji wa mbegu kwa kufufua mfumo wa matumizi ya mbegu za asili ambao wakulima wengi wanazitumia kwa kuhamasisha uhuru wa Mbegu
Alisema kuwa serikali inazitambua mbegu za asili kupitia wadau Wa mbegu za asili
Mwenyekiti wa mviwata John Safari ameiomba serikali kutambua mfumo wa mbegu usio rasimi ili wakulima wapate uhuru wa matumizi yanayokubalika kwani sheria za mbegu hapa nchini hajitambui mbegu za asili kwani zinawasidia katika kilimo na kupunguza garama za mbegu
Baadhi ya wananchi waliohudhuria maonyesho hayo ya mbegu za asili wamepongeza hatua ya kuandaa maonyesho hayo ya mbegu za asili na wameiomba serikali kuzitambua mbegu za asili na kuziwekea sheria na kuweka katika mfumo ulio rasmi kwani mbegu hizo hazitumii gharama kubwa kama mbegu nyingine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...