WAZIRI Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa amezitaka mamlaka zinazosimamia Bonde la Mto Mara kwa Nchi za Tanzania na Kenya kuwa na usimamizi madhubuti wa mazingira ya bonde la mto huo na matumizi ya rasimali katika sekta zote za kiuchumi na kijamii ili kuleta tija kwa jamii.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa Maji, Prof Makame Mbarawa amesema wananchi zaidi ya milioni mbili wanategemea kuendesha maisha yao kupitia bonde la mto Mara.

Ametaja changamoto zinazokabili sekta ya maji hususani kwa upande wa rasimali za maji kuwa ni uvamizi wa wafugaji kwenye maeneo ya vyanzo vya maji, uvamizi wa wakulima kwa ajili ya shughuli za kilimo, ukataji wa miti kwa ajili ya kuni, mkaa na ujenzi wa nyumba mjini, umwagiliaji usiokua endelevu pamoja na uhaba wa kumbukumbu na takwimu sahihi kuhusiana na vyanzo vya maji kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesema maadhimisho ya siku ya Mara mwaka huu yamefanyika kwa ufanisi mkubwa kwa kuwa mwaka huu kuliandaliwa warsha iliyojenga kueleza na kujadili changamoto na kuzitafutia ufumbuzi wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...