Anaandika Abdullatif  Yunus - Michuzi TV.
Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera imeadhimisha Wiki ya Elimu ya Watu Wazima yenye kauli mbiu isemayo "Elimu haina Mwisho' wakati ambapo jamii asilimia kubwa bado wana fikra potofu juu ya dhana ya Elimu hii, Sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Rwamishenye Bukoba Manispaa Mkoani Kagera Septemba 27 Mwaka huu.

Akizungumza Mara baada ya Kuhitimisha sherehe za Maadhimisho hayo Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba Kadole Kilugala amekiri kuwepo Kwa upotoshaji Wa dhana nzima ya Elimu ya watu wazima, wakidhani kuwa Elimu hii uhusisha wazee tu au watu wenye umri zaidi ya miaka 18, jambo ambalo sio sahihi kwani Elimu hii Kwa sasa inamgusa MTU yeyote aliyekosa Elimu na stadi za maisha kubwa ikiwa ni kujua kusoma, kuhesabu  na kuandika maarufu kama "K" tatu, Kwa utaratibu MEMKWA na MESKWA, na kuwataka wote wenye kupotosha kuacha Mara moja.
 
Kadole amesema  takwimu zinaonesha kuwa Sensa iliyofanyika  mwaka 2012 zinaonesha kuwa asilimia 22℅ ya   Watanzania  hawajui kusoma na kuandika, hivyo Serikali tayari imeanza utaratibu Wa kuwezesha programu hii kupitia mpango wa Elimu bila malipo na Kwa mara ya kwanza mwaka huu Manispaa ya Bukoba wametenga Milioni Nne kuongeza ufanisi wa Elimu hii.

Awali Afisa Elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Bukoba Mwl. Frolence Kibani amefafanua kuwa Ndani ya Wiki ya maadhimisho wameweza kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa kuwapatia Elimu wale walioikosa Elimu, wakiwemo watoto na watu wazima, sambamba na hilo Mwl. Kibani ameiomba jamii kuchangamkia vituo vinavyotoa Elimu ya watu wazima na ufundi stadi ambapo vituo hivi ni Zam zam, Nshambya Kibeta huku akisisitiza kuwa Elimu hii ni bila malipo.

Sherehe za kikomo cha wiki ya Elimu ya Watu wazima, iliyoanza 23 Septemba 2019, hizo zimepambwa na burudani mbalimbali ikiwemo nyimbo na maigizo, zikitanguliwa na maandamano yaliyoongozwa na kikundi cha ngoma kutoka shule za Adolph, huku sherehe hizo zikihudhuriwa na wadau wa Elimu, viongozi wa Taasisi mbalimbali wakiwemo wadau NMB, wanafunzi pamoja na wazazi.
 Katibu Tawala Manispaa ya Bukoba Bi. Kadole Kilugala wakati akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Elimu ya Watu Wazima.
 Afisa Elimu ya Watu wazima Bukoba Manispaa Mwl. Frolence Kibani akisoma Risala iliyoandaliwa kwa Mgeni Rasmi, Katibu Tawala kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya Bukoba, pembeni ni Msherehedhaji Mwl. Joyce Robozi.
 Katibu Tawala Manispaa ya Bukoba Bi. Kadole Kilugala wakati akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Elimu ya Watu Wazima.
 Baadhi ya Wadau wa Elimu wakiwemo watumishi Idara ya Elimu pamoja na wazazi wakiendelea kufuatilia sherehe za maadhimisho ya kilele cha wiki ya Elimu ya watu wazima.
Kati ya burudani iliyochota hisia za waliohudhuria, kutoka kwa wanafunzi wanaolelewa na Kituo cha Tumaini Education Center, ambapo hawa ni miongoni mwa watoto waliokuwa wakiishi mazingira hatarishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...