Na Said Mwishehe,Michuzi TV
SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi madhubuti wa Rais John Magufuli, imedhamiria kuhakikisha kuwa biashara za mipakani zinaimarishwa na kufanyika kwa ufanisi zaidi kwa kuondoa vikwazo vyote vya kikodi na visivyokuwa vya kikodi na kuwezesha Wananchi na Taifa kwa ujumla kunufaika na kukuza biashara.
Hayo yamesemwa leo Septemba 23 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya ambapo amerumia nafasi hiyo kuutaarifu umma na wafanyabiashara wote nchini hususan wale wanaofanya biashara mipakani.
"Wizara kwa niaba ya Serikal imeweka utaratibu maalum utakaowezesha kutoa taarifa juu ya vikwazo, changamoto au kero za kibiashara hasa zile zisizokuwa za kikodi (NTBs) wanazokumbana nazo.
"Lengo la kuweka utaratibu huu ni kuwezesha wafanyabiashara kupata huduma haraka kupitia Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali zinazotoa huduma mipakani. Kwa kuanzia, Wizara imetoa anuani maalumu za barua pepe na namba za simu za watendaji ambazo tutapenda kila mfanyabiashara anayepata vikwazo aweze kutoa taarifa kupitia namba hizo,"amesema.
Mhandisi Manyanya aidha amesema Wizara inawataka wakuu wa taasisi hizo walioko kwenye vituo vya mipakani kubandika orodha hiyo kwenye mbao za matangazo ili kurahisha mawasiliano
Ameongeza kuwa vikwazo visivyokuwa vya kikodi ni pamoja na rushwa ya kifedha na isiyo ya kifedha, urasimu na kutotoa miongozo ya taratibu zinazohitajika, kukosa taarifa muhimu na kutojua fursa zilizopo.
Amefafanua kwa upande wa Wizara, taarifa hizo zinapaswa kutumwa kwa Mratibu wa Vikwazo Visivyo vya Kiushuru (NTB’s) Aneth Simwela kupitia barua pepe tanzania@tradebarriers.org au kupiga simu katika namba +255622259341.
Amesema kwa changamoto za masuala ya Viwanda na Masoko, Wafanyabiashara na Wadau wanaweza kuwasilisha changamoto zao kupitia barua pepe dawatilamsaada@mit.go.tz au kuwasiliana na Andrew Shirima wa Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia namba ya simu +255713500532.
Pia Wizara na Taasisi ambazo zinazotoa huduma mipakani ni Mamlaka ya Mapato (TRA); Idara ya Uhamiaji, Wakala wa Vipimo (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Mkemia Mkuu wa Serikali; Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Kitengo ya Huduma za Afya ya Mimea, Idara za Maliasili na Utalii, Idara za Mifugo na Uvuvi Halmashauri za Wilaya na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
Mhandisi Manyanya amesema kiwa prodha yenye majina ya Taasisi/Mamlaka na mawasiliano ya Maafisa Wasimamizi wa Taasisi hizo kwa huduma za mipakani inapatikana kwenye tovuti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) www.tantrade.go.tz au kupitia barua pepe: info@tantrade.go.tz au feedback@tantrade.go.tz au wasiliana na Bw. John Fwalo kupitia namba ya simu +255767285252.
"Endapo hutaridhika na huduma kutoka Taasisi yeyote tajwa hapo juu, wasilisha malalamiko yako kwa barua pepe minister@mit.go.tz au ps@mit.go.tz. Unaombwa pia kutumia barua pepe tajwa endapo utaridhika na huduma zilizotolewa,"amesema Manyanya kwa niaba ya Wizara hiyo ya viwanda na biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...