Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima akizungumza na maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora wakati akifungua kikao kazi ya kuwajengea uwezo maafisa hao kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Tabora Bw. Panin Kerika akitoa neno la ukaribisho kwa Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima(wa pili kulia) wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo Maafisa Maendeleo ya Jamii na waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akielezea hali ya ukatili nchini wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo Maafisa Maendeleo ya Jamii na waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Violeth Mulyalya akielezea kuhusu wajibu wa wazazi au walezi katika malezi wakati wa wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo kuhusu Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Bi. Frida Edward akichangia mada wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Bw. Mabula Bugumba akichangia mada wakati wa wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa MAdawati ya
Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Mkoa wa Tabora wakti wa kikao
cha kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
Na Mwandishi Wetu Nzega
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii imetoa elimu kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na
Waratibu madawati ya Jinsia na Watoto mkoa wa Tabora ili kuwajengea
uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia ili kukabiliana
na vitendo vya kikatili katika jamii.
Akifungua kikao kazi cha Maafisa na Waratibu hao leo wilayani Nzega
mkoani Tabora Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii Bi. Tausi Mwilima amesema kuwa malengo ya kuwa na kikao kazi
hicho ni kuwajengea uwezo Maafisa na waratubu hao ili waweze kufikisha
elimu ya malezi na makuzi katika jamii.
Bi. Tausi ameongeza kuwa lengo la Kitini cha elimu ya malezi ya
familia ni muhimu kwani uwapa wazazi na walezi uelewa na jinsi ya
kuendeleza malezi na makuzi yenye matokeo chanja kwa watoto ili
kujenga jamii yenye kuwajibika na uzalendo.
Amesisitiza kuwa jukumu la kwanza la malezi na makuzi kwa mtoto ni la
mzazi au mlezi katika familia hivyo wazazi au walezi wana wajibu
mkubwa wa kuzingatia wanawapa watoto wao malezi na makuzi bora.
Aidha Bi. Tausi ameeleza kuwa Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto
katika Halmashauri wanajukumu kubwa kufuatilia na kuhakikisha
changamoto za malezi na makuzi zinatatuliwa katika jamii na wazazi
wanapata elimu sahihi ya kusaidia kuwajengea uelewa juu ya suala la
malezi ya familia.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Tabora Bw. Panin
Kerika amesema kuwa suala la elimu ya malezi kwa familia ni muhimu na
la msingi ambapo linasaidia katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa
Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wenye lengo
la kutokomeza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii Bw. Emmanel Burton amesema kuwa Wizara iliamua kuwa na Kitini
cha elimu ya malezi kwa familia kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya
ukatili katika familia hivyo elimu juu ya malezi na makuzi itasaidia
kupunguza vitendo vya ukatili vinavyofanywa katika familia.
Mmoja wa Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Tabora Bi.
Faiza Hassan amesema kuwa masuala ya elimu ya malezi kwa familia ni
muhimu sana kwa familia kwani familia nyingi zimekuwa zikifanya
vitendo vya kikatili bila kujua kama ni vitendo vya ukatili kwa watoto
wao.
Naye Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Uyui Bw. Godwin
Masaka amesema kuwa elimu ya malezi kwa familia itawasaidia Waratibu
wa Madawati ya Jinsia na Watoto kuwajengea uwezo wa kwenda katika
jamii kuwapatia elimu hiyo ili kuimarisha misingi ya malezi na makuzi
katika familia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...