Wateja kupata hadi riba ya asilimia 10 kwa mwaka

Watanzania watakiwa kujenga utaratibu wa kujiwekea akiba ili kuimarisha uchumi wa familia na nchi kwa ujumla ili kufikia malengo ya kujenga uchumi wa viwanda,hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Biashara wa Letshego Bank Solomon Haule alipokutana na wateja wa Bank hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya LetsGo Flexi save akaunti, akaunt ya akiba inayotoa faida ya riba hadi asilimia kumi kwa mwaka kulingana na akiba ya mteja.

"LetsGo Flexi save ni akaunti jumuishi kwasababu imezingatia na kuweka mbele maslahi ya wateja wote bila kuangalia uwezo au kipato cha mtu kupitia akaunti hii hata wateja wadogo wenye akiba chini ya shiling 20,000 watapata riba ya hadi asilimia 5% kwa mwaka."

Hafla hyo pia iliambatana na uadhimishaji wa wiki ya huduma kwa mteja ambapo Letshego Bank ilipata nafasi ya kuwashukuru baadhi ya wateja wao wanaoendelea kuwaunga mkono.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Letshego Tanzania Andrew Tarimo (aliyekaa) akimhudumia mteja katika maadhimisho ya wiki ya Wateja. Benki hiyo imezindua akaunti maalum ya Letshego Flexi ambapo wateja watapata riba ya asilimia kumi kwa mwaka kwa kuweka kiasi cha fedha cha kuanzia Tzs50, 000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...